Sinopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodios
-
Mkutano wa 9 China na Afrika, miili200 yazikwa DRC, wanafunzi 17 wateketea Kenya.
07/09/2024 Duración: 20minMakala hii imeangazia mkutano wa tisa kati ya China na Afrika huko Beijing, wafungwa zaidi ya 100 waliuawa katika gereza la makala nchini DRC, Kenya na mkasa wa moto ulivyowaua wanafunzi Kaunti ya Nyeri, uchaguzi kufanyika nchini Tunisia, na nchini Ufaransa Michel Barnier aliteuliwa kuwa waziri Mkuu, miezi miwili baada ya mvutano wa kisiasa nchini Ufaransa, na mambo mengine kwengineko duniani.
-
Kampeni ya Odinga kuwania uenyekiti tume ya AU, DRC yafungua kesi dhidi ya Rwanda
31/08/2024 Duración: 20minUzinduzi wa kampeni ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, anayegombea unyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kongamano la 74 la WHO mjini Brazzaville, nchini Congo, DRC na Kampeni inayoitwa ICC Haki kwa DRC, hali ya usalama kuendelea kuzorota nchini Sudan, shambulio la kigaidi Burkina Faso laua zaidi ya watu 300, hali nchini Israeli, na mchakato wa uchaguzi wa Marekani mwezi Novemba
-
DRC yaathirika na M-Pox, Raila asema siasa za Kenya, basi! na mengineyo
24/08/2024 Duración: 20minTumeangazia katika makala ya wiki hii ni pamoja na ugonjwa wa Mpox ulitangazwa kuwa dharura ya kimataifa, DRC ikiathirika zaidi, nchini Kenya Raila Odinga kutojihusisha tena na siasa, jeshi la Uganda lilivamia na kuharibu kambi ya kundi la waasi la LRA huko Sudan pande hasimu zasusia mkutano wa Geneva, nchini Marekani, makamu wa rais Kamala Harris akubali uteuzi wa chama chake cha Democratic kuwa mgombea wa nafasi ya urais, na mengineyo
-
Mpox yatangazwa janga la kimataifa la kiafya, mwanahabari wa Burundi Irangabiye aachiwa na mengineyo
20/08/2024 Duración: 20minMatukio ya dunia yaliyokithiri vichwa vya habari ni pamoja na virusi vya Mpox kutangazwa kuwa janga la dharura la kiafya huku bara la Afrika likiathiriwa zaidi, Burundi yamwachia mwanahabari aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10, tutaangazia siasa za Tanzania baada ya wanasiasa wa upinzani kukamatwa baadaye wakaachiwa, lakini pia hatua za mazungumzo kule Geneva kuhusu amani nchini Sudan. Pia tutaangazia mgomo wa vyombo vya habari nchini Senegal kadhalika tutachambua wito wa Umoja wa Mataifa kutaka Afrika kupewa kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja huoKule Gaza, kundi la Hamas limekataa masharti 'mpya' ya upatanishi na Israeli na mazungumzo ya kupata mkataba wa kusitisha vita hivyo, kurejelewa tena wiki hii jijini Cairo, Misri.