Jukwaa La Michezo

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:59:27
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodios

  • Uganda : Uwanja wa Namboole kuanza kutumika kwa mechi za kufuzu Kombe la dunia

    04/05/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na Uchambuzi wa orodha ya mwisho ya Kikosi cha Marathon cha Team Kenya kuelekea Olimpiki, watu watano nchini Kenya wapigwa marufuku ya muda kwa madai ya upangaji mechi. Nchini Uganda, Rais wa FUFA asema uwanja wa Naambole utakuwa tayari kuandaa mechi wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 na Ligi ya Basketboli barani Afrika mkondo wa Sahara umeanza leo.

  • KipKeino Classic: Mmarekani Kenneth Bednarek ashinda mbio za mita 100

    20/04/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia hii leo ni pamoja na matokeo ya riadha za KipKeino Classic, uchambuzi wa debi la Tanzania na Mashemeji nchini Kenya, mabondia 11 wa DRC wafuzu nusu fainali ya michuano ya African Boxing Cup, matokeo ya ligi ya basketboli Afrika mkondo wa Nile na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya

  • Olimpiki: Nigeria na Zambia zafuzu mashindano ya Olimpiki soka ya kina dada

    13/04/2024 Duración: 23min

    Kwenye makala haya utasikiliza uchambuzi wa mechi za kufuzu soka ya kina dada Olimpiki na shirikisho la riadha duniani kuwa shirikisho la kwanza kutoa tuzo za fedha, maandalizi kuelekea riadha za KipKeino Classic, mkusanyiko wa michezo DRC, uchambuzi wa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Tiger Woods na Novak Djokovic waweka historia kubwa duniani kwenye gofu na tenisi mtawalia.

página 2 de 2