Afrika Ya Mashariki

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 3:59:32
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.

Episodios

  • Juhudi za kupambana na ulawiti wa watoto katika nchi za Afrika mashariki

    09/05/2024 Duración: 09min

    Ulawiti ni janga linaloendelea kuwakumba watoto si tu katika mataifa ya ukanda wa Afrika mashariki bali katika mataifa mbalimbali ulimwenguni. Nchini Tanzania kumekuwa na takwimu za kupanda na kushuka huku baadhi ya wanaharkati wakisema kuwa swala la uzembe limekuwa likichangia kuongezeka kwa ubakaji na ulawiti kwa WatotoHatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na kuibua wito wa kitaifa kwa wazazi kuongeza ulinzi na ufuatiliaji wa watoto wao.

  • Ujumbe unaoandikwa kwenye vyombo vya usafiri katika mataifa ya Afrika

    01/05/2024 Duración: 09min

    Je ujumbe unaoandikwa unahalisia na vitu vilivyowatokea makonda na madereva wa vyombo hivyo.

  • Tanzania:Juhudi za wabunifu katika kupunguza hewa ya ukaa kutunza mazingira

    18/04/2024 Duración: 09min

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Masuala na Utalii, katika taarifa ya misitu na ufugaji nyuki inabainisha kuwa mkaa ni chanzo kikubwa cha nishati ya kaya katika maeneo ya mijini kwa kupikia na kupasha joto, kwa kuwa inachukuliwa kuwa ya bei nafuu na inapatikanakwaurahisi. Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya watu wote wa Tanzania kutegemea nishati ya majani. Nishati ya kupikia ndiyo inayoongoza kwa matumizi ya biomasi katika kaya ikilinganishwa na sekta nyingine kama vile ujenzi na kilimo sekta ya msingi.

  • Fursa za uchumi wa buluu zilizopo katika  Ziwa Victoria

    13/04/2024 Duración: 09min

    Uchumi wa Buluu ni dhana pana yenye kubeba maana nzima ya kutumia kila rasilimali itokanayo na rasilimali maji kama Bahari, mito na maziwa. Dhana hii ubeba shuguli mbalimbli ikiwemo utalii, uvuvi, kilimo cha mwani, bandari pamoja na mafuta na gesi zilizomo baharini au katika maziwa.Kwa wakazi wa Jumuiya ya Afrika mashariki hasa katika mikoa inayo zunguka Ziwa.Victoria kwa siku za usoni wanachangamkua fursa za uchumi wa buluu uliopo katika maeneo yao.Dhana hii inatafsiriwa kwa kasi kwa siku za usoni na imekuwa ikitajwa kama ndio mharobaini wakuwanusua wananchi walio wengi kutoa katika mnyonyoro wa umasikini uliotopea.

página 2 de 2