Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:52:27
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • Esneda kutoka jamii ya Yukpa asema haogopi vitisho kutetea eneo la jamii yao ya asili nchini Colombia

    15/11/2024 Duración: 03min

    Jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia imevumilia miongo kadhaa ya migogoro na watu kutawanywa inayosababishwa sio tu na mabadiliko ya tabianchi mila kandamizi bali pia kupotea kwa viumbe hai na hivyo kutishia maisha yao. Esneda Saveedra, Kiongozi wa jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia akiwa anazungumza akiketi ndani ya msitu na kando ya mto Maracas., anasema hana hofu ya kutetea ardhi hii.Ardhi anayozungumzia ni eneo hilo la mto Maracas anayotetea dhidi ya vitisho kutoka kwa waharibifu wa mazingira kufuatia yale yaliyojadiliwa katika mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa bayonuai, COP16 uliomalizika Ijumaa iliyopita huko mjini Cali nchini Colombia."Sina hofu ya kutetea ardhi hii. Yale niliyopitia kama mtoto, changamoto zote hizo, yalinipa nguvu, yalinipa ujasiri, na yakaondoa hofu yangu."Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR inatupatia taswira ya juu ya eneo la makazi ya jamii ya Yukpa, msitu mnene na kisha kwenye mto Maracas, shughuli zinaende

  • Anne Tek: COP29 isiwape kisogo wanawake wanaokabiliiwa na athari za mabadiliko ya tabianchi Afrika

    15/11/2024 Duración: 01min

    Mkutano wa 29 wa Umoja wa Mataifa wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP29 ukianza wiki ya piili mjini Baku Azerbaijan leo, wito umetolewa kwa wanawake amba oni waathirika wakubwa wa janga la mabadiliko ya tabianchi kutopewa kisogo. Anne Cheruto Tek ambaye amebeba bendera ya wanawake waathitika wa mabadiliko ya tabianchi kutoka Afrika ameiambia UN News anachokifanya COP29..“Sana sana kufuatilia haya madhara ya mabadiliko ya tabianchi hasa kwa wanawake na vijana barani Afrika. Sana sana utakuwa wanawake ndio wanaoshughulikia masuala ya maji, masuala ya kuni, masuala ya chakula , lakini mara nyingi kukiwa na janga la mabadiliko ya tabianchi kama ukame, mafuriko, wanawake ndio wanaangamia zaidi, kwa sababu wanawke ndio wanakuwa na jukumu la kuendesha nyumba na hivyo hawana nafasi ya kutafuta fedhha ambaz zinaweza kuwasaidia wakati wa majanga hayo.”Na kutokana na hayo anasema wanawake hukabiliwa na changamoto kubwa“Wengi hupata magonjwa , wengi huathhirika sana wakati wa majanga ikiwemo vifo, ukosefu wa f

  • 15 NOVEMBA 2024

    15/11/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia suala muhimu wa mabadiliko ya tabianchi tukijikita kataika mkutano wa COP29 huko Baku Azerbaijan kuwasikia wanaharakati wa mazingira kutoka nchi mbalimbali.Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 u unaofanyika Baku Azerbaijan, leo umejikita na ongezeko la gesi chafuzi ya methane ambayo kwa kiasi kikubwa inatokana na shughuli za binadamu ikiwemo ufugaji wa ng’ombe, na sasa nini kifanyike ili kuidhibiti.Tunasalia huko huko Baku, Azerbaijan. Wito umetolewa kwa wanawake ambao ni waathirika wakubwa wa janga la mabadiliko ya tabianchi wasipewe kisogo katika harakati za kuhimili na kukabili madhara ya janga hilo.Katika makala Bosco Cosmas anatupeleka Amerika ya Kusini kusikia harakati za mwanamke wa jamii ya asili za kulinda eneo lao.Mashinani leo Fathimath, kijana kutoka Maldives anatoa kauli kwa ajili ya hatua za dharura kupambana na mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa COP29.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

  • UNEP: Licha ya taarifa za ongezeko la gesi ya methane hatua zinazochukuliwa ni kidogo

    15/11/2024 Duración: 02min

    Mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP29 unaofanyika Baku Aberbaijana leo umejikita na ongezeko la gesi ya methane ambayo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na shughuli za binadamu na nini kifanyike kuidhibiti. FKulingana na ripoti iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa wa mazingira UNEP katika mkutano huo, mfumo wa teknolojia ya hali ya juu ambao unatambua uvujaji mkubwa wa gesi ya methane umewasilisha tarifa 1,200 kwa serikali na makampuni katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, lakini ni asilimia moja tu ya taarifa hizo ndizo zilizofanyiwa kazi.Ripoti hiyo mpya iliyopewa jina  “Jicho kwenye methane: Haionekani lakini inashuhudiwa” inasema licha ya ahadi zilizotolewa chini ya makubaliano ya ahadi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi ya methane kwa asilimia 30 ifikapo 2030 hatua zinazochukuliwa hazitoshelezi kupunguza gesi hiyo.Ripoti imeangazia tahadhari za methane kutoka kwenye Mfumo wa Tahadhari na hatua dhidi ya Methane

  • Jifunze Kiswahili - Ufafanuzi wa maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE”

    14/11/2024 Duración: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE” 

  • 14 NOVEMBA 2024

    14/11/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Baku kwa mkutan wa COP29, amabyo washiriki wanasaka mbinu za kujumuisha makundi yote katika harakati za kukabili na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na ongezeko la hewa chafuzi. Idhaa ya Kiswahili imezungumza na Naomi mmjoja wao kutoka Tanzania. Pata pia muhtasari wa habari na ujifunze Kiswahili.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa kisukari, shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo limesema idadi ya watu wazima wanaoishi na Kkisukari duniani ni zaidi ya milioni 8000 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara 4 tangu mwaka 1990.Baku Azerbaijan ambako mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 leo umejikita na na lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres ameainisha jukumu muhimu ambalo miji, mikoa, biashara na taasisi za kifedha lazima zitekeleze katika kuendesha juhudi za dunia nzima kufi

  • Wananchi tufahamishwe kwa kina majukumu ya MONUSCO ili kukabili habari potofu DRC

    13/11/2024 Duración: 04min

    Umoja wa Mataifa unatambua ni kwa kiasi gani habari potofu na habari za uongo kuwa ni mojawapo ya vikwazo vikuu vinavyokabili operesheni zake za  kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.  Hii imesababisha Umoja huo kuhaha kila wakati kuona ni kwa vipi itakabiliana na habari hizo, iwe ni kupitia mafunzo kwa wanahabari, au kusaidia ujenzi wa vyombo vya habari, na hata kuzungumza na wananchi. Hivi karibuni Umoja Wa Mataifa kupitia Idara yake ya Ulinzi wa Amani, kitengo cha uadilifu wa habari, ulituma Tume yake Mashariki mwa DRC kukutana na wakazi ili  kujua ni nini Umoja wa Mataifa unapaswa kufanya ili kupambana na habari potofu na za uongo nchini humo. Mwandishi wetu wa Mashariki mwa DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini, George Musubao alishuhudia ziara hiyo na ametuletea makala hii.

  • Patricia Kombo COP29: Ufadhili wa fedha utakuwa jawabu mujarabu kudhibiti mabadiliko ya tabianchi Afrika

    13/11/2024 Duración: 01min

    Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 leo ukiingia siku ya nne  mjini Baku Azerbaijan vijana kutoka Afrika wataka ufadhili uongezwe kutoka mataifa makubwa hususan yanayochangia zaidi hewa ukaa ili kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mataifa yanayoendelea ambapomiongoni mwa waathirika wakubwa ni vijana.  Asante Bosco na mmoja wa washiriki hao ni Patricial Kombo Mumbua kutoka Kenya  akiwasilisha matakwa ya vijana katika mkutano huo, na akizungumza na UN News  kuhusu ujumbe wake kwa COP29 amesema“Kwangu kama kiongozi wa vijana jambo la kwanza ni kuweza kupata zile fedha au kuzikusanya ili ziweze kusaidia mataifa ambayo yanapambana na kukabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi . Pili ni kuhakikisha kuwa viongozi kutoka mataifa ambayo yanazalisha zaidi hewa ukaa yanawajibika ili kuyafanya matifa ambayo yanaendelea kuweza kujilinda , kunufaika , kujiinua dhidi ya janga hilo na pia kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika jamii zao.”Na

  • 13 NOVEMBA 2024

    13/11/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazi ufadhili kwa wakulima huku mkutano wa COP29 ukiendelea Baku, na madhara ya mafuriko kwa wakulima nchini Sudana Kusini tukimulika jinsi Umoja wa Mataifa wanavyohaha kuwasaidia. Makala inatupeleka nchini DRC na mashinani tunasalia huko huko Sudan Kusini, kulikoni?Kuongeza kiwango cha fedha kwenye ufadhili wa miradi ya kukabili na kuhimili tabianchi nchi ikiwa ni moja ya masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan, leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bila kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi, na kuimarisha miradi ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kila uchumi duniani utakumbwa na madhara makubwa.Huko Maban, jimboni Upper Nile, kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linajenga vifaa vya kuhifadhi maji pamoja na makinga maji ili kuepusha mashamba dhidi ya mafuri

  • UNHCR Sudan Kusini yachukua hatua kupunguza madhara ya mafuriko katika sekta ya kilimo

    13/11/2024 Duración: 02min

    Huko Maban, jimboni Upper Nile, kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi ,UNHCR linajenga vifaa vya kuhifadhi maji pamoja na makinga maji ili kuepusha mashamba dhidi ya mafuriko ya msimu yanayokumba eneo hilo mara kwa mara, eneo ambalo ardhi yake ina rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Hapa shambani jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini, wakulima wakiwemo wenyeji na wakimbizi wakiwa shambani wakiimba.  Awad Usman mwenyeji wa hapa anasema kuimba kunatuliza fikra zangu. Nyimbo hazisaidii kupanda mazao, lakini zinaweza kupunguza msongo wa mawazo.Msongo wa mawazo unatokana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi yaletayo mvua kubwa na mafuriko kwenye mashamba yao.Awad anasema nakumbuka mafuriko ya mwaka 2019, yalisomba kila kitu. Ufuta wote ulisombwa. Mtama pekee ulisalia. Tulikaa ndani ya nyumba kwa siku tano, na tulipotoka tulikuta shamba zima limetwama kwenye maji.Alex Noel Kilong, afisa wa UNHCR anasema mafuriko yanaon

  • 12 NOVEMBA 2024

    12/11/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Havana Cuba amabpo Flora Nducha amaezungumza na mshiriki kutoka maitaifa mbalimbali na leo ni Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka Zimbabwe.Kuongeza kiwango cha fedha kwenye ufadhili wa miradi ya kukabili na kuhimili tabianchi nchi ikiwa ni moja ya masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan, leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bila kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi, na kuimarisha miradi ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kila uchumi duniani utakumbwa na madhara makubwa.Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyotolewa leo huko COP29 inaonesha ni kwa jinsi gani watu wanaokimbia vita, ghasia na mateso wanazidi kujikuta kwenye mazingira yaliyokumbwa na janga la tabianchi, janga ambalo

  • Kozi za Kiswahili ziongezwe ili watu wengi zaidi wajifunze duniani kote- 'Bongo Zozo'

    11/11/2024 Duración: 03min

    Kongamano la kimataifa la Kiswahili limefunga pazia mwishoni mwa wiki mjini Havana Cuba ambako washiriki takriban 400 kutoka barani Afrika, Ulaya, Asia na Aamerika wamejadiliana mada mbalimbali za kukuza na kupanua wigo wa lugha hiyo ya Kiswahili duniani. Hata hivyo wapenzi wa lujifunza lugha hiyo wanataka kozi za kujifunza Kiswahili kwa wageni ziongezwe katika sehemu nyingi zaidi ili kutoa fursa kubwa kwa wanaotaka kujifunza kama alivyobaini Flora Nducha alipozungumza na mmoja wa wachechemuzi wa lugha hiyo ya Kiswahili Nick Reynold au Bongo Zozo. Ungana nao katika Makala hii

  • Stiell: Lazima tuweke malengo ya juu ya ufadhili ili kukabili mabadiliko ya tabianchi

    11/11/2024 Duración: 02min

    Kufuatia mwaka mwingine wa viwango vya juu vya joto kali na matukio ya kupitiliza ya hali ya hewa, Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi Simon Stiell amewaeleza washiriki wa mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 , kwamba malengo mapya ya ufadhili kwa tabianchi ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa mataifa, yakiwemo yale tajiri na yenye uthabiti. Katika hotuba yake mbele ya washiriki wa mkutano huo ulioanza leo huko Baku, mji mkuu wa Azerbaijan hadi tarehe 22 mwezi huu wa Novemba, Bwana Stiell amesema kwa kadri madhara ya mabadiliko ya tabianchi yalivyo dhahiri ni lazima kukubaliana mwelekeo mpya wa ufadhili kwa miradi ya kukabili na kuhimili.Amehoji, mnataka bei za vyakula na nishati iongezeke zaidi? Je mnataka nchi zenu ziendele kushindwa kushindana kiuchumi? Je mnataka dunia yetu iendelee kukosa utulivu na kugharimu maisha adhimu?Amekumbusha kuwa janga la tabianchi linaathiri kila mkazi wa dunia kwa njia moja au nyingine.Bwana Stiell ames

  • 11 NOVEMBA 2024

    11/11/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangaziamkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29, na mradi wa lishe bora kwa watotot Afar nchini Ethiopia. Makala inatupeleka Havana Cuba na mashinani tunasalia huko huko Havana Cuba, kulikoni?Kufuatia mwaka mwingine wa viwango vya juu vya joto kali na matukio ya kupitiliza ya hali ya hewa, Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi Simon Stiell amewaeleza washiriki wa mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29, kwamba malengo mapya ya ufadhili kwa tabianchi ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa mataifa, yakiwemo yale tajiri na yenye uthabiti.Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuchagiza kaya kulima bustani za mboga za majani pamoja na ufugaji wa kuku huko jimbo la Afar, kaskazini mashariki mwa Ethiopia umesaidia familia za vijijini kukabiliana na utapiamlo miongoni mwa watoto.Makala inatupeleka Havana Cuba ambako kongamano la kimataifa ka Kiswahilii limekunja jamvi mw

  • Mradi wa UNICEF wa kuboresha lishe waleta tabasamu kwa wazazi na watoto Afar Ethiopia

    11/11/2024 Duración: 01min

    Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuchagiza kaya kulima bustani za mboga za majani pamoja na ufugaji wa kuku huko jimbo la Afar, kaskazini mashariki mwa Ethiopia umesaidia familia za vijijini kukabiliana na utapiamlo miongoni mwa watoto. Video ya UNICEF Ethiopia inaanza ikimuonesha mtoto akitabasamu, na kisha akiwa na mama yake wakielekea kwenye kituo cha afya. Mama huyu anaitwa Fatuma Kebir na mwanae huyu aliyembeba anaitwa Abdu. Fatuma anasema..“Nilihofia kuwa angeendelea kuwa na utapiamlo. Kwa hiyo nilimpeleka kituo cha afya na mhudumu wa afya akanieleza kuwa mwanangu amepoteza uzito, kama ambavyo nilihisi. Akaniambia nimlishe zaidi, hasa uji uliochanganywa na mayai, maziwa, na mboga.”Video ikimuonesha Fatuma akiandaa uji akichanganya na mayai, mtaalam wa lishe wa UNICEF, Yetayesh Maru, anasema,“Kama sehemu ya mtambuka wa hatua na uratibu dhidi ya utapiamlo kwenye jamii, Fatuma ametambuliwa kuwa ni kaya iliyo hatarini, hivyo amenufaika na mradi wa kisekta wa kuboresha

  • Tutahakikisha Kiswahili kinasambaa duniani na kusongesha ajenda za UN: Dkt. Ndumbaro

    08/11/2024 Duración: 05min

    Kongamano la kimataifa la Kiswahili leo limeng’oa nanga jijini Havana Cuba likiwaleta pamoja takribani washiriki 400 kutoka Afrika, Asia, Amerika na Ulaya ili kujadili ajenda mbalimbali za kupanua wigo wa luugha hiyo na kuitumia kuleta tija ikiwemo kusongesha malengo ya Umoja wa Mataifa kama amani na maendeleo endelevu. Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa Kongamano hilo Waziri wa utamaduni, sanaa na michezo wa Tanzania Dkt. Damas Daniel Ndumbaro amesema hili ni kongamano la kimataifa la Kiswahili na ajenda yake kuu ni kukifanya Kiswahili kivuke mipaka. 

  • 08 NOVEMBA 2024

    08/11/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea kipindi maalum kinachotupeleka jijini Havana Cubaambapo kongamano la kimataifa la Kiswahili limeng’oa nanga likiwaleta pamoja takribani washiriki 400 kutoka Afrika, Asia, Amerika na Ulaya ili kujadili ajenda mbalimbali za kupanua wigo wa luugha hiyo na kuitumia kuleta tija ikiwemo kusongesha malengo ya Umoja wa Mataifa kama amani na maendeleo endelevu.Miongoni mwa habari kubwa Umoja wa Mataifa hii leo ni uwajibikaji unasakwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya  wapalestina na waisraeli, na pia shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limeweka bayana gharama za kiuchumi na hata kiafya zilizofichika zitokanazo na mifumo ya uzalishaji, usafirishaji na ulaji wa chakula. Lakini kubwa zaidi nakupeleka Havana, Cuba kupata kwa mahtasari mazungumzo ya Flora Nducha na mmoja wa washiriki.Mashinani tunasalia huko huko Havana Cuba na fursa ni yake Profesa Juan (Huani) Jacomino (Hakumino) raia wa Cuba ambaye ni Mwalimu wa Kiswahii katia  chuo kikuu cha Havan

  • Fahamu kuhusu faida za kidiplomasia na kiuchumi zilizoletwa na lugha ya Kiswahii kisiwani Zanzibar

    07/11/2024 Duración: 06min

    Huko Havana Cuba mambo yanaendelea kuiva kwenye Kongamano la kimataifa la Kiswahili huku wageni wakitoka katika kila pembe ya dunia kushiriki. Miongoni mwao ni Waziri Tabia Maulid Mwita kutoka Zanzibar ambaye amezungumza na shuhuda wetu katika kongamano hilo Flora Nducha kuhusu faida za kiplomasia na kiuchumi zilizoletwa na lugha ya Kiswahii Kisiwani Zanzibar.

  • 07 NOVEMBA 2024

    07/11/2024 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka huko Havana Cuba kwenye Kongamano la kimataifa la Kiswahili kusikia kutoka kwa waziziri Zanzibar kuhusu faida za kiplomasia na kiuchumi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ujumbe kuhusu Kiswahili.Fedha kwa ajili ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ni jambo lililopatiwa kipaumbele katika ripoti mpya ya leo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP wakati huu ambapo kiwango cha joto kinazidi kuongezeka kila uchao na kuleta zahma duniani kote.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema hii leo watoto 6 wa kipalestina, wamesafirishwa kutoka Gaza kwenye Romania kwa matibabu mahsusi ; watatu wakiwa wanaugua saratani, wawili magonjwa ya  damu na mmoja majeraha. Wameambatana na jumla ya waangalizi 15.Na huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umezindua mfumo wa uthibitishaji, kama sehemu ya mchakato wa Luanda wenye lengo la kufuatilia m

  • Uganda imechukua hatua kuhakikisha Kiswahili kinazungumzwa shuleni hadi bungeni: Dkt. Tendo

    06/11/2024 Duración: 06min

    Kwa kutambua thamani na mchango Mkubwa wa lugha ya Kiswahili katika Kanda ya Afrika Mashariki na kimataifa,  sasa serikali ya Uganda imeivalia njuga lugha hiyo kwa kuweka mikakati maalum ya kuhakikisha inafundishwa na kuzungumzwa kuanzia shuleni hadi Bungeni. Flora Nduha wa  Idhaa hii aliyeko mjini Havana Cuba kutujuza yanayojiri katika kongamano la kimataifa la Kiswahili amebainni hayo alipozunggumza na mmoja wa washiriki kutoka nchini Uganda.

página 5 de 5