Jukwaa La Michezo

CAF: Kenya Police FC yafuzu kushiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao

Informações:

Sinopsis

Tumekuandalia mengi ikiwemo matokeo na uchambuzi wa mashindano ya COSAFA Cup inayoendelea nchini Afrika Kusini, Leopards voliboli ya ufukweni yafuzu Kombe la Dunia wakati Kinshasa yajiandaa kuandaa mechi za kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mchezo wa basketboli ya kutumia viti vya magurudumu, Kenya yateua kikosi kitakachoshiriki riadha za dunia U20 nchini Peru, tetesi za uhamisho katika vilabu vya Afrika Mashariki, Kenya Police yafuzu kombe la shirikisho barani Afrika msimu ujao. Tour de France yaanza leo nchini Italia kabla ya kurejea Ufaransa huku michuano ya EURO na Copa America ikiingia hatua za mtoano.