Habari Za Un

05 DESEMBA 2024

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani mada kwa kina inayotupeleka katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda kumulika hali ya ukatili dhidi ya wanawake kwa watu hao waliokimbia vita jinsi inavyoshughulikiwa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA leo limezindua ombi lake la kimataifa la mwaka 2025, likitafuta dola bilioni 1.4 ili kutoa huduma za afya ya uzazi zinazookoa maisha na programu muhimu za kuzuia unyanyasaji wa kijinsia kwa zaidi ya wanawake, wasichana na vijana milioni 45 kote duniani katika nchi  57 zilizoathiriwa na majanga.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo jijini Geneva, Uswisi limetangaza kutoa idhini ya awali kwa kipimo kinachoitwa Xpert® MTB/RIF Ultra dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB). Kipimo hiki pia kinaweza kupima uwezekano wa kuathiriwa kwa viuavijasumu ambacho kinakidhi viwango vya WHO.Biashara ya kimataifa inatazamiwa kufikia dola trilioni 33 mwaka 2024, kulingana na Taarifa mpya ya B