Habari Za Un

Padre Toussaint Murhula: Fikra za kikoloni zimeiharibu Afrika ni wakati wa kuziondoa

Informações:

Sinopsis

Mkutano wa mwaka 2024 wa Taaluma kuhusu Afrika leo katika leo umeingia siku ya pili hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Mkutano huo ulioandaliwa na Ofisi ya mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika UNOSAA ni wa siku tatu na umebeba maudhui "Nguvu, Haki, na watu” kwa ajili ya mabadiliko ya Afrika.Na moja ya mabadiliko ni kuondoa fikra za kikoloni tangu kufanyika mkutano wa Berlin ulioligawa mapande bara hilo  yapata miaka 140 iliyopita amesema mmoja wa washiriki wa mkutano huo aliezungumza na  Flora Nducha wa idhaa hii kuhusu kile wanachojadiliana na anaanza kwa kujitambulisha