Habari Za Un
04 DESEMBA 2024
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:57
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia uzinduzi wa ombi la ufadhili wa mahitaji ya Kibinadamu (GHO), na umuhimu wa lugha mama katika kukuza haki za binadamu. Makala tunasalia hapa makao makuu ya umoja wa mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Senegal, kulikoni?Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ikizindua Ripoti ya Kimataifa ya mahitaji ya Kibinadamu (GHO) kwa mwaka ujao wa 2025 imetangaza ombi la ufadhili kwani takriban watu milioni 305 duniani kote watahitaji msaada wa kibinadamu katika mwaka ujao.Haki si haki iwapo inatolewa kwa lugha ambayo haileweki kwa wahusika, wamejulishwa washiriki wa mkutano wa pili wa wanazuoni unaofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani na pia mtandaoni ukimulika Madaraka, Haki na Binadamu: Utawala wa Sheria na mabadiliko Afrika.Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo mkutano wa mwaka 2024 wa Taaluma kuhusu Afrika leo katika leo umeingia siku ya pili hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.