Habari Za Un

03 DESEMBA 2024

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika harakati za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kuhakikisha wafugaji kuku wasiotumia dawa kiholela wananufaika kiuchumi baada ya kupatiwa mafunzo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani ya Timor-Leste.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe mahususi kwa siku hii, ameueleza ulimwengu kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanawakumbusha kwamba ulimwengu unahitaji uongozi wa watu wenye ulemavu zaidi kuliko hapo awali. Guterres ameeleza kuwa Watu wenye ulemavu tayari wanabeba mzigo mkubwa wa majanga yanayoumiza ulimwengu lakini mara nyingi wananyimwa haki yao ya kuchangia katika suluhu za majanga haya.Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Syria hii leo imezitaka pande zinazopigana nchini Syria zifuate kikamilifu sheria za kimataifa na kuwalinda raia. Hii inatokana na ongezeko kubwa la mapigano tangu tarehe 27 mwezi uliopita ambayo yanatishia kuenea katika maeneo mengine ya