Habari Za Un
02 DESEMBA 2024
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:10:42
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia mashauriano huko Busan kuhusu matumizi ya plastiki, na ripoti ya UNODC kuhusu UKIMWI na kudhibiti dawa za kulevya katika magereza. Makala inaturejesha Havana Cuba na mashinani inatupeleka nchini Kenya, kulikoni?Vuta nikuvute kwenye mashauriano huko Busan, Korea Kusini kuhusu mkataba wenye nguvu za kisheria dhidi ya uchafuzi utokanao na matumizi ya plastiki na kulinda mazingira ya baharini imefikia ukingoni kwa mkutano kuahirishwa na wawakilishi wa nchi zilizokuwa zinashiriki kuridhia rasimu mpya yenye ibara 32 itakayojadiliwa mwakani.Wakati jana Desemba Mosi Ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya UKIMWI kwa kuhamasisha haki za binadamu ili kufanikisha vita dhidi ya ugonjwa huu hatari, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) inajivunia miaka 25 ya kujiunga na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI (UNAIDS) katika kushughulikia janga la Virusi Vya UKIMWI (VVU) miongoni mwa watu wanaotumia dawa za kulevya na miaka 20 ya kazi ya