Habari Za Un

29 NOVEMBA 2024

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika adha zinazokumba raia kwenye eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli; hakari za kukabili UKIMWI Afrika Kusini; IFAD ilivyonusuru vijana na safari za kwenda Ulaya zinazohatarisha maisha yao; Mkimbizi wa ndani Gaza anayezungumzia harakati za kusaka mkate ili kulisha familia yake.Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ofisi ya eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, Ajith Sungay amesema miezi 13 ya vita imeufanya Ukanda wa Gaza kuwa kama jehanamu, kwani kuna uharibifu usio na kifani, njaa isiyoelezeka magonjwa na kuendelea kwa mashambulizi ya mabomu yanayotawanya raia kila uchao. Flora Nducha na taarifa zaidi.Kuelekea ya Siku ya Kimataifa ya UKIMWI itakayoadhimishwa Jumapili hii, ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI (UNAIDS) iliyotolewa juzi Jumatano imeeleza kuwa dunia inaweza kufikia lengo lililokubaliwa la kukomesha UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030 lakini kwa sharti kwamba viongozi ni lazima walind