Habari Za Un

Jukwaa la UN la Muungano wa Ustaarabu limetufungua macho - Dativa Mahanyu na Mariam Mintanga

Informações:

Sinopsis

Jukwaa la 10 la Umoja wa Mataifa la Ustaarabu limekunja jamvi leo huko Cascais, Ureno ambako sambamba na jukwaa hilo, pia vijana kutoka makundi 150 duniani walikusanyika katika Jukwaa lao. Katika vijana hao walikuwemo watengeneza filamu chipukizi ambao kupitia filamu wanaeleza mambo kadha ya ulimwengu kama uhamiaji, ujumuishaji, kupambana na ubaguzi na mengine mengi. Miongoni mwa vijana hao waliohudhuria ni Dativa Mahanyu na Mariam Mintanga kutoka Tanzania. Kwanza tumsikilize Mariam Mintanga akieleza alivyojisikia kuhudhuria mkutano huu kisha tutamsikia Dativa Mahanyu akieleza kuhusu filamu ya Fid ya ambayo kupitia taasisi ya Tai Tanzania imepata tuzo ya PLURAL+