Habari Za Un

13 DESEMBA 2024

Informações:

Sinopsis

Hii leo jaridani tunaangazia hali nchini Syria, na msaada wa kibinadamu kw awakimbizi nchini Chad. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, kulikoni?Ofisi ya mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria (OSE) imesema wakati huu ikifuatilia kwa karibu hali na maendeleo nchini Syria ni muhimu kuhakikisha kwamba Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao na kwamba kuna ujumbe wa pamoja na mshikamono kuhusu hilo kutoka kwenye jumuiya ya kimataifa.Kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia Chad wakitoka Sudan kuwa ni wanawake na watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi,  UNFPA limeimarisha huduma za afya ya wanawake na watoto.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Tanzania kusikia jinsi wanafunzi wananufaika na mradi wa Umoja wa Mataifa shuleni na majumbani.Na mashinani fursa ni yake Aline kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC ambaye ni mnufaika wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula