Habari Za Un

Baada ya kunusuriwa na programu ya IOM, mhamiaji kutoka nchini Ethiopia asema katu hatorudi Yemen

Informações:

Sinopsis

Janga la kibinadamu likizidi kushika kasi nchini Yemen, shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM linaongeza kasi ya mpango wake wa kurejesha wahamiaji nyumbani kwa hiari, VHR. Mradi huu hupatia wahamiaji waliokwama njia salama ya kurejea nyumbani kwao. Kupanuliwa kwa mradi huu kunafuatia idadi ya wahamiaji nchini Yemen kuongezeka na kufikia 6,300 mwezi Oktoba mwaka huu, kwa mujibu wa mfuko wa IOM wa  Ufuatiliaji wa wahamiaji.Mwaka huu wa 2024, IOM imeshafanya safari 30 za ndege kupitia mradi huo wa VHR ikiwemo ya tarehe 5 mwezi huu waDesemba ambapo wahamiaji 175 wa Ethiopia walirejeshwa Yemen kutoka uwanja wa ndege wa Aden. Makala hii inafuatilia miongoni mwa wahamiaji hao yaliyowasibu hadi kukubali kurejea nyumbani kwa hiari. Msimulizi wako ni Assumpta Massoi.