Habari Za Un

Simfahamu baba yangu, natamani nimfahamu kwani nakosa upendo wake

Informações:

Sinopsis

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanazuiwa kutumia chakula, fedha au vitu vingine kwa ajili ya kushawishi ngono kutoka kwa mtu mwingine. Operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zinachukua hatua zaidi kuepusha ukosefu huo wa maadili , lakini bado visa hivyo vinaendelea kutokea. Katika baadhi ya matukio, watoto waliozaliwa kupitia uhusiano wa aiana hiyo wanasalia nyuma kwenye mazingira ya mizozo ambako baada ya baba zao kumaliza kuhudimia, huondoka na kubaki bila baba. Makala hii ya leo inamulika kisa kimoja cha mama na mtoto ambao wamesalia baada ya mlinda amani aliyempatia ujauzito mama husika kuondoka na kurejea nchini mwake. Msimulizi wako ni George Musubao