Habari Za Un
06 DESEMBA 2024
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:58
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika, na siku ya kimataifa ya kujitolea inayotupeleka nchini DRC. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Zambia, kulikoni?Katika kuadhimisha miaka 15 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika chini Muungano wa Afrika, Kamishna Mkuu Msaidizi wa Ulinzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Ruven Menikdiwela NA Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za Wakimbizi wa ndani Paula Gaviria Betancur wametoa kauli ya pamoja ya kupongeza Muungano wa Afrika kwa maono haya ya mbali na pia kuzisihi nchi zote barani Afrika kuutekeleza mkataba huo muhimu.Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya kujitolea kwa ajili ya amani na maendeleo, tunakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mmoja wa wafanyakazi wa kujiolea wa Umoja wa Mataifa anaelezea uzoefu wake na ni kwa nini anajivunia kufanya kazi hiyo.M