Habari Za Un

Wazazi pelekeni watoto wenu kupata chanjo dhidi ya maradhi - Bi. Halfani

Informações:

Sinopsis

Katika Wiki ya Chanjo duniani, iliyotamatishwa tarehe 30 wiki iliyopita, mtaa wa Butiama, ulioko Mtoni Kijichi katika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania ulishuhudia wazazi na walezi wakijitokeza kuwapatia watoto wao chanjo muhimu za kuwalinda dhidi ya maradhi hatari. Miongoni mwao ni  Hija Halfani ambaye alimpeleka mtoto wake mwenye umri wa siku 42 kupata chanjo yake ya kwanza. Je, ni mafanikio gani yamepatikana na kwa nini chanjo hizi ni muhimu? Ungana na Sharon Jebichii kwa makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini  Tanzania.