Siha Njema

Mzigo wa uvutaji sigara Misri ulivyo pasua kichwa kwa afya ya wengi

Informações:

Sinopsis

Misri ipo kwenye njia panda  kuhusu utekelezaji wa sheria zake za kudhibiti matumizi ya tumbaku haswa sigara na Shisha. Kwa njia moja sigara inaleta  mapato makubwa kwa mfuko wa mapato ya  serikali ya Misri ,ni tabia inayoruhusiwa ila kwa upande mwingine inakodolea macho hatari kubwa ya kiafya inayotokana na uvutaji sigara.Unapowasili Cairo jiji kuu la Misri ,ukutana na harufu tamu ya mikate ,keki na bidhaa zingine za ngano za kuokwa,marashi yanayonukia lakini pia kuna harufu ya shisha, aina ya tumbaku ya kisasa zenye ladhaa  za kupendeza lakini pia harufu kali zaidi ya sigara.Zipo sheria zinazokataza uvutaji sigara katika sehemu za umma ,shule ,vituo vya afya ila utekelezaji wake bado ni changamoto kubwa.Kuna mpango pia wa treni mwendo kasi ,maarufu Greenline ambapo uvutaji sigara umeharamishwa.Hata hivyo kibarua bado kipo cha kubadilisha mtazamo wa baadhi ya wananchi wanaoamini uvutaji sigara ni starehe ,kitu cha hadhi  na unaweza kufanya hivyo popote muradi usikamatwe.Misri pia inabidi kuangalia kwa jicho