Habari Za Un
UNICEF yawawezesha vijana kwenye kilimo nchini Kenya
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:03:09
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Kaunti ya Kirinyaga, iliyoko katikati mwa nchi ya Kenya kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, inashuhudia mageuzi mapya katika sekta ya kilimo kupitia mradi wa kuwahusisha vijana katika kilimo na lishe unaojulikana kama EKYAN. Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, na wadau nchini humo. Karibu Sabrina Saidi utupe taarifa zaidi.....(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Mradi wa EKYAN ni mfano wa ujasiriamali wa kilimo unaoongozwa na vijana, ukiwa na lengo la kutengeneza fursa za ajira, kuwanufaisha na kubadilisha maisha ya vijana walioko vijijini, kupitia mbinu bora za kilimo na lishe, ukitekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, serikali ya kaunti ya Kirinyaga na shirika linalotoa mafunzo, elimu ya biashara ndogo ndogo na uwezeshaji barani Afrika KUZA Biashara.Felista Nyakio Mutungi kijana mkulima wa kaunti ya Kirinyaga, ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo kupitia mradi huo. Na h