Habari Rfi-ki

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 3:37:54
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

Episodios

  • Africa : Ndoa zinaendelea kuvunjika haraka kinyume na awali

    17/09/2024 Duración: 09min

    Katika makala haya tunajadili misururu ya kuvunjika kwa ndoa za siku hizi  hili haliathiri tu watu wa kawaida  bali pia  watu maarufu katika jamii zetu. Je unafikiri nini kinachangia ndoa za siku hizi kuendelea kuvunjika haraka kinyume na zamani?Ndilo swali tumekuuliza, na haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Sudan Kusini : Serikali yaarisha uchaguzi kutokana na shinikizo za wadau

    16/09/2024 Duración: 09min

    katika makala haya tunajadili hatua ya serikali ya Sudan Kusini juma lililopita kutangaza kuahirisha uchaguzi mkuu uliokuwa ufanyike mwezi Desemba mwaka huu. Uchaguzi huu sasa ukisongezwa mbele kwa miaka miwili baada ya shinikizo la ndani na nje.Je huu ni uamuzi sahihi kwa Sudan Kusini?Haya hapa baadhi ya maoni yako

  • Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia chochote kile

    01/09/2024 Duración: 10min

    Kila ijumaa inapata nafasi kuchangia mada yoyoyte ndani ya makala Habari Rafiki, makala ambayo huenda hewani ndani ya rfi Kiswahili kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa. Skiza kufahamu maoni ya waskilizaji kuhusiana na mada mbalimbali.

  • Sudan : UN yatathimini kutangaza vikwazo dhidi ya majenerali wa Sudan

    29/08/2024 Duración: 09min

    Katika makala haya tunajadili hatua ya umoja wa mataifa kusema unatathimini kutangaza vikwazo dhidi ya majenerali wawili nchini Sudan ambao wamekuwa kwenye vita kwa zaidi ya miezi 17. Je unafiriki kutangazwa kwa vikwazo dhidi ya majenerali wa Sudan kutasitisha vita nchini Sudan? Unahisi jumuiya ya kimataifa imesaidia, kutatua mizozo Africa, ndio maswali tumekuuliza. Haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Kenya : Mataifa ya Africa yakosa kuzingatia katiba

    28/08/2024 Duración: 09min

    Kwenye makala ya Habari Rafiki leo tunajadili kilichofanyika nchini Kenya, ambapo taifa hilo la Africa mashariki limeadimisha miaka 14 tangu lijipatie katiba ya mwaka 2010, ila imekuwa vigumu kwa serikali kutekeleza baadhi ya vipengee vya katiba hiyo. Unafiriki nini huzuia serikali yetu kuttotekeleza  katiba?Ndilo swali tumekuuliza, na haya maoni yako.

  • Africa : Inasubiri chanjo ya Mpox kutoka ulaya

    27/08/2024 Duración: 09min

     katika makala ya Rabari Rafiki, leo mskilizaji tunajadili hatua ya Mataifa ya Afrika yalioathirika na ugonjwa Mpox kuendelea kusubiri chanjo kutoka kwa mataifa ya magharibi ili kuwapa raia walioathirika.  Je unafikiri kwa nini hadi sasa Afrika haiwezi tegeneza chanjo yake? Ndilo swali tumekuuliza na haya maoni yako.

  • Sudan : Kiongozi wa kijeshi asema yuko tayari kwa vita na hatashiriki mazungumzo ya amani

    26/08/2024 Duración: 09min

    Katika makala haya tunajadili  hatua ya kiongozi wa kijeshi nchini Sudan, kusema hataki mazungumzo yoyote yatayohusisha wapiganaji wa RSF, akisema jeshi liko tayari kupigana hata kwa miaka 100. Matamshi yake yamekuja wakati huu Marekani ikiongoza juhudi za kupata mwafaka wa mani kati yake na vikosi vya RSF.

  • Matukio ya watuhumiwa kutoroka wakiwa katika vituo vya polisi na jela

    22/08/2024 Duración: 09min
  • Juhudi za kukabili unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi

    20/08/2024 Duración: 09min

    Unyanyapaa ni hali inayowakumba watu wengi wanaoishi na virusi vya HIV katika mataifa ya ukanda.

  • Migogoro na ukosefu wa amani katika nchi wanachama za jumuia ya SADC

    19/08/2024 Duración: 09min
  • Siku ya kimataifa ya kupiga vita biashara haramu ya binadamu

    31/07/2024 Duración: 09min

    Wataalamu wanasema biashara hii haramu imekuja na mfumo mpya wa watu kusafirishwa kutafutiwa ajira katika mataifa ya kigeni.

  • Serikali ya DRC, imetangaza kuanza kuwaachia baadhi ya wafungwa kutoka katika jela zake

    29/07/2024 Duración: 10min
  • Mtazamo wa msikikilizaji kuhusu mawaziri kutoka upinzani kuunda serikali

    25/07/2024 Duración: 10min

    Rais William Ruto amependekeza viongozi wanne kutoka chama cha ODM cha Raila Odinga kuwa mawaziri Miongoni mwa viongozi hao ni Ali Hassan Joho ,John Mbadi ,Wicliffe Oparanya na Opiyo Wandayi

  • Mtazamo wa msikililizaji kuhusu maandamano Kenya iwapo yameathiri nchi zingine

    25/07/2024 Duración: 10min

    Vijana nchini Kenya wamekuwa wakiongoza maandamano dhidi ya serikali ya rais William Ruto Nchi ya Uganda imeshuhudia pia maandamano ,yanayoongozwa na vijana wa Gen Z kupinga ufisadi na maovu mengine

  • Maoni yako kuhusu matukio ya juma hili

    19/07/2024 Duración: 09min

    Kila Ijumaa rfi kiswahili inakupa nafasi kuchangia  chochote kile ambacho umeskia kwenye matangazo yetu au yale yanayoendelea hapo uliopo. Juma hili waskilizaji wetu walikuwa na maoni mseto kuhusu matukio yanayoendelea kushuhudiwa duniani. Kufahamu mengi skiza makala haya.

  • Mtazamo wa msikilizaji kuhusu kuchaguliwa tena kwa rais Paul Kagame

    19/07/2024 Duración: 10min

    Tume ya uchaguzi ya Rwanda imethibitisha Paul Kagame ni mshindi wa uchaguzi wa Julai 15 ambapo alipata asilimia 99.18 ya kura zote

  • Kenya : Polisi watuhumiwa kuwateka raia

    18/07/2024 Duración: 09min

    Tunajadili visa vya watu kutekwa nyara kuendelea kuripotiwa katika ya  mataifa yetu ya Africa hivi karibuni visa kama hivi vikiripoti kwa wingi nchini Kenya, vyombo vya usalama vikituhumiwa kwa utekaji huo. Je nchini mwako kuna visa kama hivyo ? ndio baadhi ya maswali tumeuuliza karibu Haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Kenya : Mwanaume awaua wanawake 42, nini sababu ya mauwaji haya

    16/07/2024 Duración: 09min

    Katika makala haya mshale wetu unalenga taifa la Kenya, ambapo polisi nchini humo wamefaulu kumkamata mshukiwa mkuu wa mauaji wanawake 42, ambao sehemu za miili yao iliyokuwa imekatwa vipande vipande na kuwekwa kwenye magunia kabla ya kutupwa kwenye shimo la kutupa taka. Tunauliza mskilizaji unafikiri nini huchangia mambo kama haya kutokea kwa jamii. Haya hapaa baadhi ya mano yako.

  • DRC : MONUSCO huenda ikasalia DRC kwa muda zaidi kutokana na usalama kuendelea kzuorota

    15/07/2024 Duración: 09min

    Katika makala haya tunajadili uwezekano wa vikosi vya MONUSCO nchini DRC kusalia kwa muda kwenye taifa hilo, kutokana na ripoti za uwepo wa wanajeshi wa Rwanda wanaowasaidia waasi wa M23.  Tumeuliza wewe unaunga mkono vikosi vya MONUSCO kusalia DRC? Haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Mchango wako katika taarifa zetu juma hili

    30/06/2024 Duración: 10min

    Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote ile kuhusiana na taarifa zetu au kile kinachoendelea pale ulipo. Juma hili waskilizaji walikuwa na kauli hii.

página 1 de 2