Habari Rfi-ki

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 3:59:15
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

Episodios

  • MAONI: DRC na Rwanda zitie saini makubaliano kumaliza mauaji ya raia

    20/06/2025 Duración: 10min

    Kila siku ya Ijumaa, hapa RFI Kiswahili, tunampa mskilizaji wetu nafasi kuzungumzia habari kuu ambazo tumekuwa nazo wiki hii au kutueleza jambo lolote ambalo limetokea nchini mwake. Wiki hii maoni mseto yameangazia, miongoni mwa taarifa zingine, tangazo kwamba Rwanda itatia saini makubaliano na DRC tarehe 27 Juni, kumaliza mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini pia mashambulio baina ya Israeli na Iran.

  • Burundi : Rais Ndayishimiye ataka mazungumzo na upinzani

    16/06/2025 Duración: 10min

    Rais wa Burundi Evariste #Ndayishimiye ametoa wito kwa upinzani kushiriki katika mazungumzo na chama chake CNDD-FDD baada ya uchaguzi wa wiki iliyopita ambao ulikumbwa na upinzani mkubwa kwa ukosefu wa uwazi.   Hata hivyo upinzani haujaonyesha nia ya kushiriki mazungumzo hayo. Tunakuuliza, ni sahihi upinzani kujiunga na serikali ? skiza makala haya kuskia maoni ya mskilizaji.

  • Utumwa wa watoto waendelea kuripotiwa licha ya juhudi mbalimbali zinazowekwa

    13/06/2025 Duración: 09min

    Juni 12, ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Watoto. Inakadriwa, takriban watoto milioni 200 kote duniani wanatumikishwa badala ya kuwa shuleni.   Tunakuuliza, serikali yako inafanya vya kutosha kukomesha utumwa wa watoto? Unamfahamu mtoto anayefanyishwa kazi?

  • Kwa nini wanaume wanashindwa kutafuta ushauri wa afya ya akili

    13/06/2025 Duración: 10min

    Makala haya yanaangazia afya ya akili, ikizingatiwa kuwa Juni ni Mwezi wa Uhamasishaji wa Afya ya Akili ya Wanaume.   Unafikiri ni kwanini wanaume wanashindwa kutafuta ushauri wa afya ya akili? Unadhani afya ya akili ya mwanaume inasahaulika? Skiliza makala ya leo usikie maoni kutoka kwa waskilizaji wetu.

página 2 de 2