Jua Haki Zako

Tume ya haki za binadamu nchini Uganda yatuhumiwa kuegemea upande wa serikali

Informações:

Sinopsis

Makala haya yanaangazia tendekazi wa tume za kutetea haki za biandamu za serikali zetu za Africa mashariki.Hii ni baada ya lalama kutoka kwa kiongozi wa upinznai nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine kwamba tume ya haki nchini Uganda imekuwa ikiegemea upande wa serikali katika kutekeleza majukumu yake.  Robert Kyagulanyi,amelazimika kuondoa lalama zake mbele ya tume ya haki ya kutetea haki za biandamu nchini Uganda kutokana na madai inayosema  tume hiyo imeshindwa kuyashughulikia.Wine alikuwa amewasilisha kesi yake mwaka 2018 akilalamikia hatua ya polisi nchini Uganda kukiuka haki zake kwa kumzuia kuandaa tamasha za muziki zaidi ya 20, mbali na polisi kuchukuwa nyombo vyake vya mziki, hili akidai lilimzuia kupata haki yake ya kupata mapato kutokana na mrengo wake wa kisiasa. Fahamu mengi kwa kuskiza makala haya.