Sinopsis
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episodios
-
DRC : Haki ya wanawake kupata elimu
05/11/2024 Duración: 10minNchini DRC, kumeripotiwa upungufu wa watoto wa kike katika kupata elimu, hili likidaiwa kuchangiwa na tamaduni zilizopitwa na wakati. Katika makala haya basi Butua Balingane, mkurugezi wa chuo kikuu cha walimu cha ISP, Goma ambaye anasimulia masaibu anayopitia mtoto wa kike nchini DRC kupata elimu. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
-
Kenya : Wanawake 97 wauawa kwa kipindi cha miezi tatu
05/11/2024 Duración: 09minNchini Kenya, idara ya polisi imekiri kwamba wanawake 97 wameuawa kwa kipindi cha miezi 3, baadhi miili yao ikipatikana imenyofolewa. Ni visa ambayo vimesababisa viongozi wa ngazi ya juu akiwemo rais William Ruto, ambaye ametoa agizo wa asasi za uchunguzi nchini humo kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika visa hivyo. Kwenya makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Kenya, ambapo mtaalamu wa maswala ya jamii bi Carolina Situma anaeleza nini kimechangia mauwaji haya.
-
Kenya : Visa vya raia kutekwa yaongezeka
25/10/2024 Duración: 09minNchini Kenya, visa vya raia kutekwa na kisha baadaye kuachiliwa au kupatikana wameuawa vinazidi kuongezeka, visa kadhaa vikiendelea kugonga vichwa vya habari. Katika Makala haya George Ajowi angaazia visa hivi na jinsi mkuu wa polisi nchini Kenya alikosa kufika mahakamani kueleza walipokuwa baadhi ya wakenya waliotekwa.
-
Hatua zilizopigwa katika kumuinua mtoto wa kike
24/10/2024 Duración: 10minKatika muendelezo wa makala kuhusu siku ya mtoto wa kike duniani, tunaangazia vyanzo vya visa vya unyanyasaji wa watoto wa kike na hatua zilizopigwa na mashirika mbalimbali katika kuifanya sauti ya mtoto wa kike kusikika.
-
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani
18/10/2024 Duración: 09minSiku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Oktoba, ni fursa ya kuangazia changamoto zinazokabili watoto wa kike duniani na kukuza usawa wa kijinsia. Katika mwaka 2024, mada ilikuwa "Kutoa sauti kwa watoto wa kike: Fursa na Changamoto katika Utu wa Kike."Makala haya yataangazia kwa kina haki za mtoto wa kike na hatua zilizopigwa katika kusababisha mtoto wa kike kuskizwa na hata hatua zilizochukuliwa ili kuboresha elimu, afya, na usalama wa watoto wa kike, pamoja na jinsi jamii zinaweza kushiriki katika kuwasaidia kufikia ndoto zao.Aidha, itajadili umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wazazi katika kufanikisha malengo haya.
-
MAMILLIONI YA WATU HASA WATOTO BARANI AFRIKA HAWAJAPATA HAKI ZA CHAKULA
16/10/2024 Duración: 09minChakula ni muhimu kwa maisha, kuishi, heshima, ustawi, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa watu binafsi, jamii, na mataifa. Sheria za kimataifa zinatambua haki ya kila mtu kupata chakula cha kutosha na haki ya kuwa huru kutokana na njaa. Haki hii ni ya msingi kwa utekelezaji wa haki zote za binadamu. Nchini Kenya, ni haki ya kikatiba, iliyoko katika Kifungu cha 43(1)(C) kinachosema: "Kila mtu ana haki ya kuwa huru kutokana na njaa na kuwa na chakula bora na cha kutosha .Lakini je, sheria hii inatambuliwa ? Je, watu wanaelewa haki yao ya chakula? Na hali ya usalama wa chakula nchini Kenya iko vipi leo?Katika kipindi cha leo ,cha jua haki zako , tunaangazia iwapo watu wanapata haki zao za kupata chakula na jinsi changamoto za kiuchumi na kimazingira zinavyoathiri upatikanaji wa chakula nchini Kenya
-
DRC : Wanawake wabakwa katika gereza la Makala nchini
19/09/2024 Duración: 09minKatika makala haya tunaangazia ripoti ya umoja wa mataifa kusema kwamba zaidi ya wanawake wafungwa ya 260 walibakwa katika jela ya Makala nchini DRC, mapema mwezi huu wakati wa jaribio la wafungwa kutoroka jela. Ripoti hiyo imebaini kwamba kati ya wafungwa 348 katika gereza hilo la Makala, wafungwa 268, walitendewa vitendo vya unyanyasaji wa kingono ikiwemo ubakaji, wanawake 17 kati ya waliobakwa wakiwa chini ya umri wa miaka 19.Ripoti hiyo aidha imeongeza kuwa wanawake hao walilazimika kutafuta mbinu za kuzuia magonjwa baada ya kutendewa vitendo hivyo vya kikatili.Awali serikali ya DRC ilikuwa imekiri kubakwa kwa wanawake hao ila haikotoa idadi ya wanawake waliobakwa.Kadhalika ripoti hiyo pia imesema wafungwa 129 waliojaribu kutoroka jela waliuawa kwa kupingwa risasi, katika gereza hilo la Makala ambao linastahili kutoa huduma kwa wafungwa 1500, ila lina zaidi ya wafungwa alfu 15.Rais Felix Tshisekedi aliagiza kufanyika kwa uchuguzi kuhusiana na jaribio hilo la wafungwa kutoka, na mikakati ya kupunguza idad
-
Kenya : Watoto wateketea shuleni, je jukumu la nani kumlinda mtoto akiwa shuleni
16/09/2024 Duración: 09minNchini Kenya zaidi serikali inaendesha uchunguzi wa chembechembe za DNA, za wanafunzi 21 wa shule ya msingi ya Endatasha baada yao kuteketea kiasi ya kutotambulika, kabla ya miili yao kutolewa kwa familia. Miili limewaacha wazazi kwenye njia panda wasijue la kufanya, wakati huu maswali yakiendelea kuulizwa je nani wakulaumiwa baada ya mkasa huo wa moto shuleni. Kufahamu mengi skiza makala haya.
-
Kenya: Vikundi vya kina mama vyajitokeza kupinga ukeketaji
27/08/2024 Duración: 10minKatika makala haya tunajikiti kuangazia uketetetaji ambapo wasichana wamekuwa ukiendelea kukeketewa nchini Kenya licha ya serikali kanzisha kampeni ya kuhamasisha umma kuhusu athari zinazotokana na ukeketaji huo. Jamii za Kenya, kupitia kwa kina mama na wasichana waliopitia ukeketaji kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii wameanzisha vikundi vya kutetea haki za wasichana ili kuwalinda kutokana na ukeketaji huo. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
Kenya : Jamii za mipakani zataka serikali kuwapa vitambulisho
24/08/2024 Duración: 09minJamii zinazoishi mikapani nchini Kenya kwa muda zimekuwa zikikosa huduma muhimu ya kupata vitambulisho kutoka na sababu ambazo wenyewe wanasema serikali inawabagua. Katika makala haya tunajikiti kuangazia masaibu ya jamii za mipakani nchini kenya kupata vitambulisho. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
Kenya : Mawikili watoa mafunzo ya sheria kwa vijana
17/08/2024 Duración: 09minMawakili mjini Mombasa pwani ya Kenya wamenza kutoa mafunzo ya sheria kwa vijana waliokuwa wakiandamana kushinikiza mabadiliko. Mawakili hao ambao ni wanachama wa chama cha mawakili nchini LSK, wamesema hatua hiyo imechochewa na maandamano yaliokuwa ya vijana maarufu kama Gen-Z leo lengo lao kuu likiwa kuwawajibisha viongozi serikalini. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya
-
Tanzania : Human Right Watch lasema Tanzania inawahangaisha raia wa Ngorongoro
06/08/2024 Duración: 10minKatika makala haya saba yetu inalenga taifa la Tanzania eneo la Ngorongoro ambapo serikali imekuwa ikiwahamisha wenyeji eneo hilo, ili kuihifadhi eneo hilo kutokana na historia yake. Tuangazia repoti ya shirika la kimataifa la kutete haki za biandamu la Human Watch ambayo imetuhumu serikali ya Tanzania kwa kuwafurusha kwa nguvu mamia ya raia wa kimasaai kutoka eneo la Ngorongoro, maafisa wa wanyama pori wakidaiwa kuwahangaisha kwa kuwapiga wenyeji ili kuwafurusha kutoka katika ardhi za mababu zao.Karibu kwenye makala haya utaskia kutoka kwa wadau mbalimbali huku tukijadili ripoti hii ya Human Right Watch.
-
Kenya : Haki za wanawake pamoja na kina dada wanaojiuza
03/08/2024 Duración: 10minKatika makala haya tunajadili haki za kina dada pamoja na kina dada wanaojiuza. Nchini Kenya, kina dada wanaojiuza pia wanataka kutambuliwa.
-
Kenya : Haki ya wanahabari kuteleza majukumu yao bila vikwazo
27/07/2024 Duración: 09minJuma hili tunaangazia haki za wanahabari kupeperusha habari zao bila kuingiliwa na vyombo vya usalama katika mataifa yao. Shaba yetu bila shaka inalenga taifa la Kenya, nchi ambayo wanahabari wamejeruhiwa wakati wakitekeleza majukumu yao, ya kuangazia maandamano ya vijana wa Gen Z, ambao wamekuwa wakishinikiza mabadiliko nchini Kenya. Kwa siku sasa kilio cha wanahabari nchini Kenya kimekuwa ni kutaka serikali kuheshimu haki zao kwa kuwaruhusu kutekeleza wajibu wao bila vikwazo.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
Kenya : Polisi wa Uingereza watuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu
16/07/2024 Duración: 09minKatika makala haya tunaangazia dhuluma zinazodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa Uingereza ambao wana kambi ya mazoezi nchini Kenya leo la Nanyuki. Wanajeshi hao wanadaiwa kuwabaka na kuwaua wanawake mbali na kuwacha vilipuzi katika maeneo ya mazoezi ambavyo baadaye hulipuka na kusababisha majiraha na maafa. Wanawake wambao wamekuwa na uhusiano wa kimapaenzi na wanjeshi wa uingreza eneo hilo la Nanyuki wamesumulia namna gani wamesalia na majiraha ya moyo kutokana na kuachwa na wapenzi wao wa kizungu ambao baada ya mazoezi yao, wao hurejea nchini mwao licha ya kuwazalisha.
-
Kenya : Wanaume wanapitia dhuluma za kijinsia kwenye ndoa, ila wamesalia kimya
10/07/2024 Duración: 09minVisa vya dhuluma dhidi ya wanawake vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara katika jamii mbalimbali barani Afrika na hata duniani,jambo ambalo limechangia sheria nyingi kuanzishwa kulinda wanawake,lakini hata hivyo dhuluma hizo zimeanza kuwakumba wanaume wengi kwa kunyanyaswa na kupingwa na wake wao. Katika makala haya tunaangazia dhuluma za kijinsia dhidi ya wanaume shaba yetu ikilenga taifa la Kenya, ambapo mwanahabari wetu Victor Moturi alitangamana na wanaume ambao wamehangaishwa na kudhulumiwa kwenye jamiii nchini Kenya hasa eneo la Magharibu. Kufahamu mengi skiza makala haya.
-
Sudan Kusini inakabiliwa na hali ya binadamu kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi
06/07/2024 Duración: 09minTaifa la Sudan Kusini linashuhudia wimbi kubwa la wakimbizi wanaoendelea kukimbia vitra nchini Sudan, licha taifa hilo kuendelea kushuhudia changamoto nyingi tu ikiwemo ukosefu wa amani katika baadhi ya majimbo yake. katika makala haya tunazama kuangazia ripoti ya shirika la Care in South Sudan ambayo imechangia ripoti kuhusiana na hali ya binadamu nchini Sudan Kusini. Kufahamu mengi skiza makala haya.
-
Kenya : Haki ya raia kuandamana kufikisha ujumbe kwa serikali
25/06/2024 Duración: 09minNchini Kenya vijana wamekuwa wakiandamana kulalamikia kile wataja mpango wa serikali kuongeza kodi kwa kutumia mswada wa fedha wa mwaka 2024. Idadi kubwa ya vijana hao wanapinga mswaada huo wanaosema utaongeza gharama ya maisha kipindi hiki wengi wao wakiwa tayari hawana ajira, makali ya gharama ya maisha nayo yakiendelea kulemaza shughuli zao za kila siku.Maandamano hayo yameandliwa na kundi la vijana linalojiita Gen Z, yaani kizazi cha vijana waliozaliwa kati ya mwaka 1995 hadi 2010.Vijana hawa wanadai serikali ya rais William ruto imeanza kuwa dhalimu kwa kuongeza ushuru kwa bidhaa muhimu kama vile soda za wanawake na vinengnevyo. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi
-
Amnesty International : Adabu ya kifo imeongezeka zaidi duniani
18/06/2024 Duración: 10minIdadi ya watu waliopewa adabu ya kifo iliongezeka zaidi mwaka 2023, mataifa ya mashariki ya kati na nchini Somalia abadu hiyo ikiripotiwa kuwa ya juu zaidi. Kwa mjibu wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, katika ripoti yake ya kila mwaka, zaidi ya watu 1, 153 walipewa adabu ya kifo mwaka 2023 pekee, bila kujumuisha idadi kutoka nchini China, taifa ambalo linaripotiwa kuwa msiri katika kutoa taarifa kama hizi. Idadi hii ni asilimia 30 zaidi ikilinganishwa na mwaka 2022. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
Kenya : Haki za watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi wanataka kutambuliwa zaidi
17/06/2024 Duración: 09minKatika makala haya ni awamu ya pili tunaendelea na mazungumzo yetu na bwana meshaka Sisende raia wa Kenya anayeishi na ulemavu wa ngozi. Juma lililopita tuliangazia pakubwa changamoro wanazopitia raia hawa naoishi na ulemavu wa ngozi na hapa tunazidi kuangazia mananikio ya raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi.Miaka kadhaa iliopita mauwaji ya raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi yalikithiri sana nchini Tanzania, hatua iliochangia viongozi wa tabaka mbalimbali kusimama kidete kukemea mauwaji hayo mamlaka nazo zikiwakamata waliokuwa wakihusishwa na mauaji hayo kwa misingi ya kishirikiana. Ni hapo ndipo wasanii kama vile Herbert Naktare maarufu Nonini kutoka nchini Kenya aliachilia wimbo wake wa Colour Kwa Face, kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwakumbatia watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.