Jua Haki Zako

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 3:56:54
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Episodios

  • Kenya : Wanaume wanapitia dhuluma za kijinsia kwenye ndoa, ila wamesalia kimya

    10/07/2024 Duración: 09min

    Visa vya dhuluma dhidi ya wanawake vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara katika jamii mbalimbali barani Afrika na hata duniani,jambo ambalo limechangia sheria nyingi kuanzishwa kulinda wanawake,lakini hata hivyo dhuluma hizo zimeanza kuwakumba wanaume wengi kwa kunyanyaswa na kupingwa na wake wao. Katika makala haya tunaangazia dhuluma za kijinsia dhidi ya wanaume shaba yetu ikilenga taifa la Kenya, ambapo mwanahabari wetu Victor Moturi alitangamana na wanaume ambao wamehangaishwa na kudhulumiwa kwenye jamiii nchini Kenya hasa eneo la Magharibu. Kufahamu mengi skiza makala haya.   

  • Sudan Kusini inakabiliwa na hali ya binadamu kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi

    06/07/2024 Duración: 09min

    Taifa la Sudan Kusini linashuhudia wimbi kubwa la wakimbizi wanaoendelea  kukimbia vitra nchini Sudan, licha taifa hilo kuendelea kushuhudia changamoto nyingi tu ikiwemo ukosefu wa amani katika baadhi ya majimbo yake. katika makala haya tunazama kuangazia ripoti ya shirika la Care in South Sudan ambayo imechangia ripoti kuhusiana na hali ya binadamu nchini Sudan Kusini. Kufahamu mengi skiza makala haya.

  • Kenya : Haki ya raia kuandamana kufikisha ujumbe kwa serikali

    25/06/2024 Duración: 09min

    Nchini Kenya vijana  wamekuwa wakiandamana kulalamikia kile wataja mpango wa serikali kuongeza kodi kwa kutumia mswada wa fedha wa mwaka 2024. Idadi kubwa ya vijana hao wanapinga mswaada huo wanaosema utaongeza gharama ya maisha kipindi hiki wengi wao wakiwa tayari hawana ajira, makali ya gharama ya maisha nayo yakiendelea kulemaza shughuli zao za kila siku.Maandamano hayo yameandliwa na kundi la vijana linalojiita Gen Z, yaani kizazi cha vijana waliozaliwa kati ya mwaka 1995 hadi 2010.Vijana hawa wanadai serikali ya rais William ruto imeanza kuwa dhalimu kwa kuongeza ushuru kwa bidhaa muhimu kama vile soda za wanawake na vinengnevyo. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi

  • Amnesty International : Adabu ya kifo imeongezeka zaidi duniani

    18/06/2024 Duración: 10min

    Idadi ya watu waliopewa adabu ya kifo iliongezeka zaidi mwaka 2023, mataifa ya mashariki ya kati na nchini Somalia abadu hiyo ikiripotiwa kuwa ya juu zaidi. Kwa mjibu wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, katika ripoti yake ya kila mwaka, zaidi ya watu 1, 153 walipewa adabu ya kifo mwaka 2023 pekee, bila kujumuisha idadi kutoka nchini China, taifa ambalo linaripotiwa kuwa msiri katika kutoa taarifa kama hizi. Idadi hii ni asilimia 30 zaidi ikilinganishwa na mwaka 2022. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

página 2 de 2