Jua Haki Zako

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 3:58:31
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Episodios

  • Kenya: Wayu Daba wapokeahati miliki ya shamba

    23/09/2025 Duración: 09min

    Katika makala haya  tunaangazia hatua ya kihistoria kwa jamii ya wafugaji nchini Kenya. Jamii ya Wayu Daba imekabidhiwa rasmi hati miliki ya ardhi yao kupitia Mpango wa Kusimamia Ardhi Kidigitali, unaoendeshwa na serikali  mradi unaotekelezwa kwa ushirikiano na Shirika la Chakula na Kilimo, FAO. Hati hii inaguza maeneo makubwa ya ardhi, ikiwemo ardhi loevu yenye rutuba, misitu ya kiasili yenye wanyama na mimea adimu, pamoja na maliasili zinginezo ambazo zimekuwa nguzo ya maisha ya jamii hiyo kwa vizazi vingi Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Africa : Haki ya waandishi wa vitabu

    19/09/2025 Duración: 10min

    Katika makala haya  tutajadili haki za mwandishi wa vitabu, Je, mwandishi wa kitabu ana haki gani anapochapisha kitabu chake katika mashirika ya uchapishaji? Ni kipi kinafaa kuzingatiwa katika mchakato wa uchapishaji? Maswali haya yote yanamzunguka mwandishi, mchapishaji na shirika la uchapishaji ili kuibuka na mwafaka katika tasnia ya uandishi. Na ndiyo baadhi ya mambo yanayojadiliwa kwenye makala haya.

  • Maandiko matakatifu yapewe nafasi kusuluhisha mizozo

    17/09/2025 Duración: 10min

    Katika makala haya tunaangazia safari ndefu ya amani katika mataifa yanayopitia migogoro, Shabaha ikiwa ni Sudan Kusini na Somalia. Mataifa haya yamepitia miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mizozo ya kisiasa, na changamoto za kiusalama ambazo zimeathiri mamilioni ya raia wao.  Lakini katikati ya changamoto hizo, mashirika mbalimbali ya kimataifa na ya kikanda yamekuwa mstari wa mbele kusukuma gurudumu la amani. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Mashambulizi kupitia mitandao ya kijamii

    02/09/2025 Duración: 09min

    Mitandao ya kijamii na teknolojia za kidijitali zimekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Tunawasiliana, tunajifunza, tunafanya biashara na hata kushiriki mijadala ya kitaifa kupitia mitandao. Lakini pamoja na manufaa haya, kumekuwa pia na changamoto kubwa: mashambulizi ya maneno, udukuzi wa akaunti, na hata ulaghai wa kifedha. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Je mchango wa wanawake ni upi katika juhudi za kupigania haki zao

    29/08/2025 Duración: 09min

    Wanawake wametuhumiwa kwa kukosa kupigania haki zao, lakini msimamo huu unakanusha na wengi. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Dunia: watoto wanazidi kutumika kama vijakazi

    23/08/2025 Duración: 10min

    Mwezi wa Juni ulishuhudia matukio mawili muhimu ya kimataifa yakiangazia haki na ustawi wa watoto. Mnamo tarehe 12 Juni, dunia iliadhimisha Siku ya kupinga Ajira ya Watoto, (World Day Against Child Labor) ikirejelea takwimu za kutisha kwamba watoto milioni 160 duniani kote bado wamenaswa katika ajira ya watoto - wengi wakifanya kazi chini ya mazingira hatarishi. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Africa : Mazingira yanavyoathiri haki za watoto

    22/08/2025 Duración: 09min

    Katika makala haya tunangazia uharibifu wa mazingira unavyoathiri haki za  watoto. Skiza makala haya kufahamu zaidi.

  • Kenya : Haki ya kumiliki ardhi ya jamii ya wafugaji

    22/08/2025 Duración: 10min

    Jamii za wafugaji nchini Kenya, bado zinapitia changamoto za kumiliki ardhi, jamii hizo ni kama vile,Turkana, Samburu, Rendille, Borana, Gabra na nyingine , zimeathiriwa kwa muda mrefu na unyang’anyi wa ardhi wakati wa ukoloni, ambao uliendelezwa hata baada ya uhuru . Licha ya kutambuliwa kwa haki za jamii katika Katiba ya 2010 na kupitishwa kwa Sheria ya Ardhi ya Jamii ya mwaka 2016, jamii hizi bado zinakumbwa na changamoto za ardhi,unyang’anyaji wa mashamba na ukosefu wa haki za  kisheria—hali inayotishia siyo tu maisha yao bali pia utamaduni.

  • EAC : Uhuru na haki ya wanahabari kujiunga miungano

    30/07/2025 Duración: 09min

    Kataika makala haya  tunajadili umuhimu wa wanahabari kuelewa na kulinda haki zao, hasa kupitia vyama na miungano ya waandishi wa habari. Katika mazingira ambapo uhuru wa habari uko mashakani, na waandishi wengi wanakumbwa na changamoto kazini, je, kuna msaada wowote wa pamoja? Ni moja tu ya maswali tunayatarajia kuyajibu kwenye makala ya haya. Skiza makala haya kufahamu mengi

  • EAC : Wakimbizi wazidi kukimbia makwao wakitafuta amani

    28/07/2025 Duración: 10min

    Maelfu ya watu kote barani Afrika wanalazimika kuyahama makazi yao—wengine kwa sababu ya vita, wengine kwa sababu ya mateso au hali ngumu ya maisha.   Wanakimbilia nchi jirani wakitafuta usalama, hifadhi, na matumaini ya kuanza upya, lakini safari ya kuwa mkimbizi si rahisi, ni safari ya maumivu, vizingiti, na kupoteza mengi. Katika makala haya tunajadili visingiti wanavyokumbana navyo watu wanaokimbia maakazi yao kutokana na vita.   Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Kenya : Haki ya mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa

    17/07/2025 Duración: 09min

    katika makala haya mskilizaji tunazAma kuangazia  uamuzi wa kihistoria uliofanywa hivi majuzi na Mahakama ya juu zaidi ya Kenya kuhusu haki za mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ya dini ya Kiislamu—hasa kuhusu haki ya kurithi mali ya baba yake. Uamuzi huu umetangazwa kuwa hatua muhimu katika mapambano ya kuhakikisha kila mtoto anaheshimiwa na kulindwa kikatiba bila kujali dini au mazingira ya kuzaliwa kwake. Kwa miongo mingi, baadhi ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa, hasa katika jamii za Kiislamu, wamekuwa wakinyimwa haki ya kurithi mali ya baba zao moja kwa moja  kwa mujibu tamaduni ya dini hiyo.   Kufamu mengi skiza makala haya.

  • Maziwa Makuu : Haki ya afya ya akili

    15/07/2025 Duración: 10min

    Afya ya akili ni nguzo ya kila mmoja wetu ili kuafikia haki nyingine muhimu. Benson Wakoli alifanya mazungumzo na bi Ann Maria Qwicha, mwanahabari na mtetezi wa haki za binadamu hasa afya ya akili ili kufahamu mengi zaidi katika mapambano haya ya kuhakikisha afya ya akili inalindwa.

  • Kenya : Vijana wazidi kuandamana

    01/07/2025 Duración: 09min

    Kwa wiki za hivi karibuni zimekuwa za misukosuko nchini Kenya, mitaa ya jiji la Nairobi na miji mingine mikuu imekuwa ikifurika vijana… wakiwa na mabango mikononi, miili yao ikiwa tayari kwa chochote — hata kwa  gesi ya kutoa machozi  na risasi. Lakini maandamano haya yanamaanisha nini? Vijana hawa wanadai nini? Na wanaruhusiwa kisheria kufanya hivyo? Ndio maswali tutakayokuwa tunayajibu kwenye makala haya.   Karibu katika makala ya Jua Haki Zako – makala ambayo siku zote hukuelemisha kuhusu haki zako tena za msingi jina langu ni benson Wakoli

  • EAC : Haki za wanawake maeneo ya vita

    24/06/2025 Duración: 09min

    Katika kila kona ya dunia, sauti za wanawake zimekuwa zikipigania jambo moja kuu – haki. Haki ya kusikilizwa,  Haki ya kuthaminiwa, Haki ya kupewa nafasi sawa. Na hapa Africa Mashariki  ingawa hatua zimepigwa, safari ya mwanamke kuelekea usawa bado ina changamoto, katika hali ya vita kama vile, Mashariki mwa DRC, nchini Sudan Kusini na kaskazini, kaskazini mwa Ethiopia na pia Musumbiji. Skiza makala haya kufahamu juhudi zinafanywa na shirika la Women For Women kutetea haki za wanawake kwenye maeneo ya vita, licha misaada kupunguzwa.

  • DRC : Haki ya wanawake Mashariki mwa DRC

    23/06/2025 Duración: 10min

    Katika makala haya  tunajikita kuangazia hali ya haki ya wanawake Mashariki mwa DRC baada waasi wa M23 kufaulu kudhibiti miji ya Goma na Bukavu. Tunazungumza na wakili Maggie Mkulima Shukru kutoka jijini Bukavu kutueleza hali ilivyo mashariki mwa DRC. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Kenya: Haki ya matumizi ya vyombo vya dijitali

    10/06/2025 Duración: 10min

    Kadri Afrika inavyozidi kuingia katika ulimwengu wa  kidijitali, kila siku mamilioni ya watu wanaingia mitandaoni—kutafuta taarifa, kuwasiliana, kufanya biashara na hata kushiriki mijadala ya kisiasa. Lakini swali kuu ni Je, watu wote wanaelewa haki zao katika mazingira haya mapya ya kidijitali? Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Kenya : Haki ya wanaume na wanawake

    03/06/2025 Duración: 10min

    Kwenye makala haya tunaendeleza mahojiano yetu na Njeri mwangi mwanaharakati wa kutetea haki za kijisia Njeri mwangi Skiza makala Kufahamu mengi

  • Kenya : Harakati za kutetea jinsia

    31/05/2025 Duración: 10min

    Nchini Kenya, harakati za kutetea njisia inazidi kushika moto mwanaharakati Njeri Mwangi, akiendelea kuhamasisha raia. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Amnesty International : Saudi Arabia inawanyanyasa wafanyakazi wa nyumbani

    23/05/2025 Duración: 09min

    Shirika la Amnesty International imeitaka serikali ya Kenya pamoja na ile ya Saudi Arabia kushiriiana na kuweka mikakati ya kuhakikisha haki za raia wa Kenya wanaofanya kazi katika mataifa ya Ugaibini hazitatiziki. Katika ripot iyake Amnesty imesema kuwa wanawake wanaofanya kazi za nyumbani huko Uarabuni wanapitia mateso za kijinsia, kunyanyashwa kimapato na hata kuuawa.

  • Kenya : Demokrasia inavyotafsiriwa Africa

    18/05/2025 Duración: 09min

    Katika makala haya tunazama kuangazia swala zima la demokrasia na uhusiano wake na haki za binadamu.Unavyofahamu mskilizaji demokrasia mara nyingi hotofautiana na mazingira ya nchini mbalimbali duniani. Mara kadhaa swala demokrasia limehusishwa na haki za binadamu, katika makala haya Benson Wakoli anajadili swala hili na muasisi wa shirika la utafito la Afro barometer Jane Wanga ambaye pia ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Nairobi kufahamu uhuasiano uliopo kati ta demokrasia na haki za binadamu.

página 1 de 2