Jukwaa La Michezo

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:59:27
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodios

  • Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei azikwa kwa heshima kamili za kijeshi

    14/09/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia hii leo ni mkusanyiko wa uchambuzi na matokeo ya mechi za kufuzu AFCON 2025, mechi za klabu bingwa Afrika kufuzu awamu ya makundi, washindi wa riadha za Diamond League, matokeo ya lLigi ya basketboli ya Afrika U18, droo ya AFCON U20 ukanda wa CECAFA, ligi za ukanda na ulaya pamoja na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya msimu mpya utakaoanza wiki ijayo

  • AFCON 2025: Safari ya kuelekea Morocco yaanza kwa mataifa ya Afrika

    07/09/2024 Duración: 24min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo na uchambuzi wa mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2025, kifo cha mwanariadha wa Uganda nchini Kenya, matokeo ya Zurich Diamond League, matokeo ya U18 Afrobasket na Congo Cup, uchambuzi wa matokeo ya  mataifa ya Afrika kwenye Olimpiki ya walemavu jijini Paris, mechi za Ligi ya Mataifa ya Ulaya na tuzo za Ballon D'Or mwaka 2024

  • Mashindano ya Tong IL Moo Do, Mombasa Open yafutiliwa mbali kutokana na ufadhili

    31/08/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya kufuzu klabu bingwa kwa kina dada, uchambuzi wa vikosi vya timu za Afrika Mashariki na kati kuelekea mechi za kufuzu AFCON 2025, matokeo ya riadha ya Rome Diamond League na riadha za dunia U20, mashindano ya Tong IL Moo Do Mombasa Open kufutiliwa mbali, matokeo ya Olimpiki ya walemavu na uhamisho wa wachezaji ulaya.

  • Mashindano ya kimataifa, Mombasa Open Tong IL Moo Do 2024 yacheleweshwa kwa wiki

    24/08/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchambuzi wa mechi za kufuzu klabu bingwa Afrika, riadha za Diamond League, FIBA Afrobasket kwa kina dada, hatma ya mashindano ya Mombasa Open Tong IL Moo Do mwaka huu, unachostahili kujua kuhusu Olimpiki ya walemavu inayoanza wiki ijayo jijini Paris huku kiungo Ilkay Gundogan akirejea klabuni Man City.

  • Namna wanariadha wa Afrika walivyopokelewa kutoka Olimpiki ya Paris

    17/08/2024 Duración: 24min

    Jumamosi hii tumezungumzia namna wanariadha wa Afrika walivyopokelewa na mataifa yao kutoka Olimpiki ya Paris, michuano ya klabu bingwa Afrika imeanza kusaka tiketi ya hatua ya makundi, uhamisho tata wa wachezaji wa soka nchini Kenya huku ligi za Afrika Mashariki na Ulaya zikianza kurejea, Mbappe ashinda taji la kwanza Real Madrid, Pochettino kuwa kocha wa Marekani

  • Paris Olimpiki: Tamirat Tola kutoka Ethiopia ndiye mshindi wa mbio za marathon

    10/08/2024 Duración: 19min

    Tuliyokuandalia Jumamosi hii kutoka taasisi ya Alliance Francaise, ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya marathon, riadha na mashindano mengine ya Olimpiki ya Paris yaliyotukia wiki hii. Pia tunaangazia fainali kubwa zinazosubiriwa jioni ya leo na kesho asubuhi kwenye marathon ya kina dada lakini pia kifo cha aliyekuwa rais wa tano wa shirikisho la soka Afrika CAF, Issa Hayattou.

  • Jukwaa La Michezo: Fainali ya mita 100 kwa wanaume yasubiriwa, Olimpiki Paris

    04/08/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo ya Olimpiki hapo jana raia wa St Lucia Julien Alfred akishindia taifa lake medali ya kwanza ya Olimpiki, Sudan Kusini yaaga mashindano ya basketboli kibingwa, uchambuzi wa wanariadha wa Afrika Mashariki wanaotarajiwa kushiriki nusu fainali na fainali kadhaa leo usiku na kesho, uchambuzi wa mechi za nusu fainali ya soka lakini pia kwenye mjadala tunazungumzia kashfa ya jinsia ya mabondia Angela Carini na Imane Khelif

  • Jukwaa La Michezo: Cheptegei aishindia Uganda medali ya kwanza Olimpiki ya Paris

    03/08/2024 Duración: 23min

    Joshua Cheptegei ashinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 10,000 huku Malkia Strikers ikibanduliwa mashindanoni. Morocco na Misri zafuzu nusu fainali huku waafrika kwenye uogeleaji wakifanya vibaya. Pia tutakufahamisha matokeo ya judo, basketboli, kuendesha basikeli na jedwali la medali ambapo Uchina inazidi kuongoza jedwali hilo

  • Paris Olimpiki: Ufaransa yashinda dhahabu ya raga, Kenya ikimaliza nambari tisa

    28/07/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya Olimpiki na mjadala kuhusu wanariadha wanaotarajiwa kung'ara kwenye Olimpiki wiki ijayo riadha zitakapoanza pamoja na matokeo ya Toyota Cup Yanga ikiilaza Kaizer Chiefs huku George Russel akishinda mkondo wa Belgian GP kwenye mashindano ya langalanga.

  • Olimpiki ya Paris: Mambo muhimu ya kujua kuhusu mashindano ya mwaka huu

    20/07/2024 Duración: 17min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na mambo muhimu unahitaji kujua kuhusu Olimpiki  ya mwaka huu kabla ya kuanza, uchambuzi wa fainali ya CECAFA Kagame Cup kati ya APR ya Rwanda na Red Arrows ya Zambia, tetesi za uhamisho Afrika Mashariki n aUlaya pamoja na matokeo ya Tour de France ikielekea ukingoni huku kocha wa Uingereza Gareth Southgate akijiuzulu kuifunza timu ya taifa ya wanaume.

  • Timu ya Kenya yaanza kuwasili Miramas, Ufaransa tayari kwa Olimpiki

    13/07/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na droo ya hatua ya awali kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao, matokeo ya Monaco Diamond League, Team Kenya yaanza kuwasili Ufaransa tayari kwa Olimpiki, matokeo ya CECAFA Kagame Cup na tetes iza uhamisho pamoja na uchambuzi wa fainali ya EURO, Copa America na fainali za tenisi kwenye Wimbledon.

  • Shirikisho la soka barani Afrika CAF latangaza droo ya michuano ya kufuzu AFCON 2025

    06/07/2024 Duración: 23min

    Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya mwaka 2025, fainali ya Cosafa Cup, mipango ya Team Kenya kuelekea Olimpiki ya mwaka huu, uchambuzi wa mechi za robo fainali michuano ya Euro na Copa America, raia wa Eritrea Girmay Hailu Biniam ashinda hatua ya nane ya Tour de France wakati kocha wa Manchester  United Erik ten Hag aongeza mkataba wake. 

  • CAF: Kenya Police FC yafuzu kushiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao

    29/06/2024 Duración: 23min

    Tumekuandalia mengi ikiwemo matokeo na uchambuzi wa mashindano ya COSAFA Cup inayoendelea nchini Afrika Kusini, Leopards voliboli ya ufukweni yafuzu Kombe la Dunia wakati Kinshasa yajiandaa kuandaa mechi za kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mchezo wa basketboli ya kutumia viti vya magurudumu, Kenya yateua kikosi kitakachoshiriki riadha za dunia U20 nchini Peru, tetesi za uhamisho katika vilabu vya Afrika Mashariki, Kenya Police yafuzu kombe la shirikisho barani Afrika msimu ujao. Tour de France yaanza leo nchini Italia kabla ya kurejea Ufaransa huku michuano ya EURO na Copa America ikiingia hatua za mtoano.

  • CAF yatangaza tarehe mpya kwa michuano ya AFCON na WAFCON 2025

    22/06/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo ya riadha za Afrika nchini Cameroon, matokeo ya tenisi ya Davis Cup nchini Angola, bondia wa DRC Christophe Mputu ashinda medali ya 70, watu 13 wapigwa marufuku nchini Uganda kwa visa vya upangaji mechi, Ons Jabeur na Aryna Sabalenka kukosa Olimpiki kuzingatia afya yao.

  • Kipyegon, Omanyala wafuzu Olimpiki ya Paris kwenye mchujo wa kitaifa

    15/06/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na mchujo wa kitaifa wa Kenya kuteua timu itakayowakilisha kwenye Olimpiki ya Paris mwaka huu, Kenya yakosa kupandishwa daraja kwenye tenisi mashindano ya Billie Jean King Cup, uwanja wa Amahoro nchini Rwanda umeidhinishwa na FIFA kuandaa mechi za kimataifa, Junior Starlets ipo guu moja kufuzu Kombe la Dunia, droo ya kufuzu AFCON 2025 kuandaliwa Julai na michuano ya EURO kuanza Ujerumani. 

  • French Open: Iga Swiatek ashinda ubingwa wake wa nne wa Roland Garros

    08/06/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchambuzi wa mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 (Afrika), Kenya kuandaa mashindano ya mchujo kutafuta timu itakayowakilisha katika Olimpîki ya Paris mwezi Julai huku wanamichezo 33 wakipigwa na marufuku kwa kutumia dawa za kusisimua misuli, matokeo ya Congo Cup, kocha Gamondi arefusha mkataba wake klabuni Yanga huku zikiwa zimesalia siku sita kabla ya mashindano ya EURO nchini Ujerumani, Iga Swiatek ashinda ubingwa wake wa nne wa French Open

  • BAL2024: Petro de Luanda yaibuka na taji la Ligi ya Basketboli barani Afrika

    01/06/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa fainali ya Ligi ya Basketboli Afrika mwaka huu, matokeo ya Diamond League mkondo wa Oslo na mchujo wa raga duniani, uchambuzi wa vikosi vya Afrika Mashariki na Kati kuelekea mechi za kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2026, uchambuzi wa Fainali ya Klabu bingwa Ulaya (Dortmund dhidi ya Real Madrid) na matokeo ya French Open huku Ronaldo akitokwa na machozi baada ya kupoteza fainali ya Saudi Kings Cup

  • DRC: Sebastian Desabre arefusha mkataba wake kama kocha wa timu ya taifa

    25/05/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa fainali ya Klabu bingwa Afrika, Tanzania waibuka na kombe la shule za upili afrika mchezo wa soka, fainali za ligi ya basketboli kuanza nchini Rwanda wakati makocha wa Kenya na Uganda wataja vikosi vyao kufuzu Kombe la Dunia na matokeo ya Ligi za ulaya.

  • CAF: Nani ataibuka na taji la Klabu bingwa barani Afrika 2024?

    18/05/2024 Duración: 24min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2024, Zanzibar kuandaa fainali za mashindano ya shule za upili barani Afrika, Mkusanyiko wa michezo kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, Maniema yarejea kwenye mashindano ya vilabu barani Afrika, uchambuzi wa mbio za kuwania taji la Uingereza kati ya Man City na Arsenal, Ngolo Kante arejea kikosini mwa Ufaransa, Brazil yateuliwa kuandaa Kombe la Dunia la kina dada la mwaka 2027.

  • Diamond League: Mary Moraa na Beatrice Chebet waibuka washindi riadha za Doha DL

    11/05/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia hii leo ni pamoja na matokeo ya riadha kwenye Doha Diamond League, AFCON UAE kuanza hapo kesho huko Dubai, michuano ya Congo Cup, uchambuzi wa mechi za Ligi ya Basketboli ya Afrika, Guinea yafuzu fainali za Olimpiki kwenye soka, mechi za kufuzu Kombe la Dunia la U17 kwa kina dada, Mbappe atangaza rasmi kuondoka PSG na uchambuzi wa fainali za mwaka huu za michuano ya bara Ulaya.

página 1 de 2