Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:50:09
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • 25 SEPTEMBA 2025

    25/09/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum inayomulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa UNGA80, na tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi.Wakati viongozi wa nchi na serikali wanahutubia wakiwa ndani  ya jengo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas ujumbe wake kwa UNGA80 ameutoa kwa njia ya video iliyorekodiwa kutokana na kutopata kibali cha kuingia Marekani. Katika hotuba hiyo amesisitiza kuwa, Ukanda wa Gaza utaendelea kuwa sehemu ya Taifa la Palestina na tuko tayari kuwajibika kikamilifu kwenye uongozi na usalama wa eneo hilo. Hamas hawatokuwa na jukumu lolote kwennye utawala.”.Mapema kabla ya Palestina, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, alihutubia wajumbe akitaka nchi wanachama kujitolea upya kwa misingi ya usawa, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa. Amesema hilo ni muhimu kwa kuwa “wakati ambapo hapo awal

  • Taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu - Volodymyr Zelenskyy

    24/09/2025 Duración: 03min

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu wanachoweza kufanya ni kutoa matamko makali pekee na kwamba kwa sasa duniani sheria pekee za Kimataifa haziwezi kusaidia nchi kujilinda bila ya kuwa na silaha pamoja na marafiki wenye nguvu wa kukusaidia. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.

  • ECSA: Diplomasia ya kisayansi kutumika kusongesha Mkataba wa Zama Zijazo Afrika

    24/09/2025 Duración: 07min

    Katika siku ya pili ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, kando ya hotuba, viongozi wa nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA watakuwa na mkutano wa kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya, baada ya kujifunza kutokana na COVID-19 au UVIKO19. Mkurugenzi Mkuu wa ECSA Dkt. Ntuli Kapologwe akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ametaja wanachotarajia kwenye mkutano huo..

  • 24 SEPTEMBA 2025

    24/09/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia hotuba ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika siku ya pili ya mjadala mkuu wa UNG80, na ujumbe wa washiriki wa mkutano huu kutoka Nigeria na Tanzania.Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu wanachoweza kufanya ni kutoa matamko makali pekee na kwamba kwa sasa duniani sheria pekee za Kimataifa haziwezi kusaidia nchi kujilinda bila ya kuwa na silaha pamoja na marafiki wenye nguvu wa kukusaidia.Katika siku ya pili ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, kando ya hotuba, viongozi wa nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA watakuwa na mkutano wa kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya, baada ya kujifunza kutokana na COVID-19 au UVIKO19.Tukisalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Mjadala Mkuu wa UNGA80 mbali ya kusikiza hotuba za viongozi unaambatana na mamia ya matukio na mikutano ya kando.

  • Wasichana vigori hawapaswi kusahaulika - Mwanaharakati Yejide Aina

    24/09/2025 Duración: 02min

    Tukisalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Mjadala Mkuu wa UNGA80 mbali ya kusikiza hotuba za viongozi unaambatana na mamia ya matukio na mikutano ya kando. Leo, sauti kutoka pande zote za dunia zinaitaka haki ya kijamii katika moja ya mikutano ya kando na miongoni mwa sauti hizo ni ya  mwanaharakati na mhamasishaji wa masuaa ya wasichana kutoka Nigeria ambaye anasema wasichana vigori hawapaswi kusahaulika. Flora Nducha anatujuza zaidi

  • 23 SEPTEMBA 2025

    23/09/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum na mada yetu inamulika maoni kuhusu miaka 80 ya Umoja wa Mataifa. Pia tunakuetea muhtasari wa habari unaofuatilia ujumbe wa viongozi katika mjadala mkuu wa UNG80.viongozi wa dunia wamekutana leo hapa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ikiwa ni siku ya kwanza ya Mjadala Mkuu wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ukiambatana na vikao vya kando vya ngazi ya juu. Katika hotuba yake ya UNGA 80 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa dunia kufanya maamuzi “ni aina gani ya dunia tunataka kujenga pamoja.”Kuanza kwa UNGA maana yake idadi kubwa ya wageni, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UN anayeshughulikia habari na teknolojia, Bernardo Mariano, amesema wamejipanga kutoa huduma ya internet (Wi Fi) kwa watu 40,000 huku wakihakikisha hotuba za viongozi zinapeperushwa bila hitilafu za kiufundi wala kuvurugwa na mashambulizi ya mtandaoni.Na Hapo kesho Jumatano viongozi wa jumuiya ya Afya ya nchi za Afrika Mashariki, Kati

  • UN waadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake

    22/09/2025 Duración: 04min

    Umoja wa Mataifa hii leo umeadhimisha miaka 80 tangu kusainiwa kwa Mkataba wake tarehe 26 Juni 1945, tukio lililotoa matumaini mapya kwa dunia iliyokuwa imechoka kutokana na vita kuu mbili za dunia, mauaji ya halaiki na ukoloni. Katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kumbukizi ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa ni fursa ya kukumbuka ujasiri wa waanzilishi wa taasisi hiyo na kuimarisha mshikamano wa kimataifa katika kukabili changamoto zinazokabili dunia hivi sasa. Tuungane na Leah Mushi aliyefuatilia maadhimisho hayo atupatie taarifa zaidi.

  • Tumefika hapa UN, tafadhali tusikilizeni - Emily Mohohlo

    22/09/2025 Duración: 02min

    Kando ya maadhimisho ya siku ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, hapa makao makuu kumefanyika mashauriano ya faragha yenye lengo la kusaka majawabu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mashauriano ya leo ni sehemu ya mashauriano 10 yatakayofanyika kuelekea mkutano wa tabianchi wa wakuu wa nchi na serikali utakaofanyika keshokutwa Jumatano hapa Umoja wa Mataifa. Assumpta Massoi amezungumza na mmoja wa watoa mada kwenye mashauriano hayo ambayo matokeo yake yatawasilishwa kwenye mkutano wa viongozi. Kwako Assumpta.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Nats..Katika uwanda wa wageni nje ya jengo la mikutano nakutana na Emily Mohohlo, Mratibu wa shirika la kiraia la Slum Dwellers International kutoka Afrika Kusini linalojikita katika kuhakikisha maeneo ya mabanda mijini yanakuwa jumuishi, yana mnepo na maisha yao yanaboreshwa.Nikamuuliza umuhimu wa mkutano na kusema..(Sauti ya Emily Mohohlo)“Mkutano huu ni muhimu kwangu kwa sababu katika maisha halisia kuna joto kupindukia na linasababisha vifo kwa wanawake na pia kutoweka kw

  • 22 SEPTEMBA 2025

    22/09/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa washirirki ya mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, hasa maadhimisho ya miaka 80 ya umoja huo. Pia tunamulika mashauriano ya faragha yenye lengo la kusaka majawabu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi.Umoja wa Mataifa hii leo umeadhimisha miaka 80 tangu kusainiwa kwa Mkataba wake tarehe 26 Juni 1945, tukio lililotoa matumaini mapya kwa dunia iliyokuwa imechoka kutokana na vita viwili vya dunia, mauaji ya halaiki na ukoloni. Katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kumbukizi ya kuanzishwa kwa UN ni fursa ya kukumbuka ujasiri wa waanzilishi wa taasisi hiyo na kuimarisha mshikamano wa kimataifa katika kukabili changamoto zinazokabili dunia hivi sasa.Tukisalia na maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa , moja ya mchango mkubwa unaotoa kwa dunia tangu ulipoanzishwa mwaka 1945 ni kusaidia mamilioni ya watu wanaolazimika kufungasha virago kukimbia makwao na kuwa wakimbizi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita. Uganda

  • Asante UN lakini msichoke kusaka amani ya DRC: Mkimbizi Uganda

    22/09/2025 Duración: 04min

    Wakati dunia ikiadhimisha miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, moja ya mchango mkubwa unaotoa kwa dunia tangu ulipoanzishwa mwaka 1945 ni kusaidia mamilioni ya watu wanaolazimika kufungasha virago kukimbia makwao na kuwa wakimbizi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita. Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi maelfu ya wakimbizi wengi kutoka Sudan, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakisaidiwa chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mengine. John Kibego kutoka Radio washirika Kazi-Njema FM iliyoko mjini Hoima Uganda amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wakimbizi hao akielezea mchango mkubwa wa Umoja wa Mataifa kwake. Kwako Kibego.

  • Amri ya kuhama 'kaa la moto' kwa WaPalestina Gaza

    19/09/2025 Duración: 03min

    Baada ya amri iliyotolewa na jeshi la Israel la kuwataka Wapalestina walioko katika eneo la mji wa Gaza huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel kuondoka eneo hilo kwani linataka kufanya mashambulizi, hali imekuwa mbaya kwa wananchi hususan wazee ambao sasa wanafunga safari kilometa nyingi kuondoka eneo hilo. Leah Mushi anatujuza masahibu wanayo kumbana nao watu hao.

  • Balozi Lokaale: Licha ya changamoto  hakuna taasisi mbadala wa UN duniani

    19/09/2025 Duración: 02min

    Ilikuwa miezi, wiki na sasa imesalia siku tatu tu kabla ya mjada mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 kun’goa nanga hapa kwenye Makao Makuu jijini New York Marekani ambapo viongozi wa Dunia na wakilishi mbalimbali watashiriki kwenye mkutano wa 80 wa Baraza Kuu. Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa. Flora Nducha ameketi na mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ekitela Lokaale kuzungumzia Afrika na Umoja wa Mataifa katika miaka na umuhimu wa Umoja huo duniani, hiki ni kionjo tu cha maohojiano hayo akianza na mchango wa Afrika Umoja wa Mataifa

  • 19 SEPTEMBA 2025

    19/09/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa ndani wa Palestina Gaza, na ujumbe wa mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ekitela Lokaale kuhusu mchango wa Afrika katika kazi za Umoja wa Mataifa. Pia tunakwenda Tanzania kumulika amani.Baada ya amri iliyotolewa na jeshi la Israel la kuwataka Wapalestina walioko katika eneo la mji wa Gaza huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel kuondoka eneo hilo kwani linataka kufanya mashambulizi, hali imekuwa mbaya kwa wananchi hususan wazee ambao sasa wanafunga safari kilometa nyingi kuondoka eneo hilo.Ilikuwa miezi, wiki na sasa imesalia siku tatu tu kabla ya mjada mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 kun’goa nanga hapa kwenye Makao Makuu jijini New York Marekani ambapo viongozi wa Dunia na wakilishi mbalimbali watashiriki kwenye mkutano wa 80 wa Baraza Kuu. Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa.Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani, hapo Jumapili tarehe 21 mwe

  • UN Tanzania yatoa elimu ya amani na utangamano kwa wanafunzi kuelekea

    19/09/2025 Duración: 02min

    Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani, hapo Jumapili tarehe 21 mwezi Septemba 2025, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na baadhi ya wadau nchini humo, umeendesha warsha ya siku moja ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Hazina jijini Dar es Salaam kuhusu ya umuhimu wa kuishi kwa amani na kuchukua hatua sasa katika kuidumisha. Warsha hiyo imeongozwa na kauli mbiu  “Chukua hatua Sasa, kwa ajili ya Dunia yenye Amani.” Katika warsha hiyo, baadhi ya wanafunzi wameeleza walichojifunza na namna elimu hiyo inavyoweza kuwanufaisha katika maisha yao ya kila siku. Shuhuda wetu katika mafunzo ni Sabrina Saidi anatupasha ilivyokuwa

  • Tathmini ya miaka 30 ya harakati za kusongesha haki za wanawake - Balozi Mwongella

    18/09/2025 Duración: 07min

    Jumamosi hii hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu masuala ya wanawake, tathmini ya miaka 30 ya harakati za kusongesha haki za wanawake. Sasa Sabrina Said amezungumza na aliyekuwa Katibu Mkuu wa mkutano huo Balozi Gertrude Mongella kupata tafakuri yake katika katika makala hii.

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya methali "MZOEA PUNDA HAPENDI FARASI"

    18/09/2025 Duración: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "MZOEA PUNDA HAPENDI FARASI"

  • 18 SEPTEMBA 2025

    18/09/2025 Duración: 10min

    Jaridani leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kuhusu masuala ya wanawake, tathmini ya miaka 30 ya harakati za kusongesha haki za wanawake na utamsikia maoni ya Balozi Gertrude Mongella kutoka Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza Jumatatu ijayo, Rais wa Mkutano huo Annalena Baerbock  amewaambia waandishi wa habari jijini New York, Marekani kuwa “jukumu letu ni Umoja wa Mataifa uwe thabiti kwa miaka 80 ijayo. Michakato ya kuhakikisha hilo ndio itakuwa jukumu letu mwaka huu, ikiwemo kusongesha ajenda ya marekebisho ya Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo tukitaka Umoja wa Mataifa thabiti, basi tunahitaji ahadi kutoka serikali zote duniani.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayotolewa kila mwaka kabla ya kuanza kwa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu inasema Umoja wa Mataifa umeendelea kusimama imara, ukifanya kazi ya kuendeleza amani, kuchochea maendeleo endelevu, na kupunguza mateso ya kibinadamu licha ya majari

  • Agizo jipya la kuhamisha watu katika ukanda wa Gaza ni ‘msumari wa moto kwenye kidonda’

    17/09/2025 Duración: 03min

    Wakati Israeli ikiwa imetoa amri mpya ya watu kuhama kutoka jiji la Gaza katika eneo inalokalia kimabavu la Palestina, na kuelekea eneo ililotenga na kuliita ukanda wa kibinadamu kusini mwa Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limesikitishwa na agizo hilo jipya ikisema eneo halina ukubwa wala huduma za kutosha kusaidia wale walioko tayari huko, sembuse wale watakaowasili. Huduma za afya ni tete kama anavyosimulia Flora Nducha kwa taarifa hii. 

  • UNDP Zambia: Ukulima kupitia miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi

    17/09/2025 Duración: 01min

    Kupitia mradi wa SCRALA uliowezeshwa na  shirika la Umoja wa Mataifa  la mpango wa maendeleo, UNDP, wakulima wadogo nchini Zambia sasa wanaweza kulima mwaka mzima kwa kutumia miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi kama vile mifumo ya umwagiliaji na vituo vya ukusanyaji mazao, jambo linalochangia kuongezeka kwa tija na upatikanaji wa masoko. Sheila Jepngetich anasimulia zaidi.

  • 17 SEPTEMBA 2025

    17/09/2025 Duración: 09min

    Jaridani leo jaridani tunaangazia haki ya elimu kwa wasichana na wanawake nchini Afghanistan, na kuzorota kwa huduma za afya katika ukanda wa Gaza. Pia tunakwenda nchini Zambia kumulika mradi wa wakulima wadogo.Tarehe kama ya leo, 18 Septemba mwaka 2021 dunia ilishitushwa na kuhuzunishwa na tangazo lililotolewa la uongozi wa Taliban nchini Afghanistan la kukataza wasichana barubaru kuendelea na masomo na kwamba darasa la sita ndio mwisho wa elimu yao. Sasa ni miaka minne na katazo hilo bado limesimama kitu ambacho Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa ni “moja ya dhulma kubwa za wakati wetu.”Wakati Israeli ikiwa imetoa amri mpya ya watu kuhama kutoka jiji la Gaza katika eneo inalokalia kimabavu la Palestina, na kuelekea eneo ililotenga na kuliita ukanda wa kibinadamu kusini mwa Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limesikitishwa na agizo hilo jipya ikisema eneo halina ukubwa wala huduma za kutosha kusaidia wale walioko tayari huko, sembuse wale watakaowasili. Huduma za afya ni tete.Kupiti

página 1 de 5