Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
Sasa tunalima mboga shuleni na nyumbani - Wanafunzi Buhigwe Tanzania
13/12/2024 Duración: 03minKupitia mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP, awamu ya Pili, Shule ya Msingi Buhigwe, iliyoko wilayani Buhigwe, mkoa wa Kigoma, ilipatiwa mafunzo kupitia Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), likishirikiana na asasi isiyo ya kiserikali RECODA. Mafunzo haya yalilenga mbinu bora za kilimo ambapo wanafunzi waliweza kuanzisha bustani za mboga kupitia somo la Elimu ya Kujitegemea. Mradi umeanza kutekelezwa na matunda yanaanza kuonekana kama asimuliavyo Assumpta Massoi kwenye makala hii.
-
UNFPA yasambaza huduma muhimu ya ukunga kwa wakimbizi wa Sudan nchini Chad
13/12/2024 Duración: 01minKutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia Chad wakitoka Sudan kuwa ni wanawake na watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA limeimarisha huduma za afya ya wanawake na watoto kama anavyosimulia Selina Jerobon.
-
13 DESEMBA 2024
13/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia hali nchini Syria, na msaada wa kibinadamu kw awakimbizi nchini Chad. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, kulikoni?Ofisi ya mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria (OSE) imesema wakati huu ikifuatilia kwa karibu hali na maendeleo nchini Syria ni muhimu kuhakikisha kwamba Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao na kwamba kuna ujumbe wa pamoja na mshikamono kuhusu hilo kutoka kwenye jumuiya ya kimataifa.Kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia Chad wakitoka Sudan kuwa ni wanawake na watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA limeimarisha huduma za afya ya wanawake na watoto.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Tanzania kusikia jinsi wanafunzi wananufaika na mradi wa Umoja wa Mataifa shuleni na majumbani.Na mashinani fursa ni yake Aline kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC ambaye ni mnufaika wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula
-
UN: Lazima kuhakikisha Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao
13/12/2024 Duración: 01minOfisi ya mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria (OSE) imesema wakati huu ikifuatilia kwa karibu hali na maendeleo nchini Syria ni muhimu kuhakikisha kwamba Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao na kwamba kuna ujumbe wa pamoja na mshikamono kuhusu hilo kutoka kwenye jumuiya ya kimataifa. Flora Nducha na taarifa zaidi.
-
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi maana ya neno MIDABWADA
12/12/2024 Duración: 28sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno MIDABWADA”
-
12 DESEMBA 2024
12/12/2024 Duración: 10minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa ikiangazia wanawake na wasichana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambapo ukatili wa kingono ni jinamizi linalowakumba kila uchao kutokana na mapigano yanayoendelea kwenye eneo hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno MIDABWADA.Leo si siku ya kimataifa ya huduma za afya kwa wote mwaka huu ikibeba mudhui “Huduma za afya kwa wote ni jukumu la serikali” yakisisitiza kwamba Uwekezaji katika huduma za afya kwa wote UHC, unaimarisha usawa na uwiano wa kijamii na pia unanufaisha uchumi wa taifa kwa kuboresha afya na ustawi, kuongeza ushiriki wa wafanyikazi na tija, na kujenga mnepo kwa watu, familia na jamii.Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syri Geir O. Pedersen leo amesema “Picha kutoka kwenye magereza ya Sednaya na vituo vingine vya kizuizini nchini Syria vinadhihirisha unyama na ukatili usiofikirika ambao Wasyria wamevumilia na umekuwa ukiripotiwa kwa miaka mingi.”Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yuko z
-
Baada ya kunusuriwa na programu ya IOM, mhamiaji kutoka nchini Ethiopia asema katu hatorudi Yemen
11/12/2024 Duración: 04minJanga la kibinadamu likizidi kushika kasi nchini Yemen, shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM linaongeza kasi ya mpango wake wa kurejesha wahamiaji nyumbani kwa hiari, VHR. Mradi huu hupatia wahamiaji waliokwama njia salama ya kurejea nyumbani kwao. Kupanuliwa kwa mradi huu kunafuatia idadi ya wahamiaji nchini Yemen kuongezeka na kufikia 6,300 mwezi Oktoba mwaka huu, kwa mujibu wa mfuko wa IOM wa Ufuatiliaji wa wahamiaji.Mwaka huu wa 2024, IOM imeshafanya safari 30 za ndege kupitia mradi huo wa VHR ikiwemo ya tarehe 5 mwezi huu waDesemba ambapo wahamiaji 175 wa Ethiopia walirejeshwa Yemen kutoka uwanja wa ndege wa Aden. Makala hii inafuatilia miongoni mwa wahamiaji hao yaliyowasibu hadi kukubali kurejea nyumbani kwa hiari. Msimulizi wako ni Assumpta Massoi.
-
UNICEF nchini Rwanda kwa kushirikiana na UNICEF Switzerland na Liechtenstein wafanikisha ‘kinesitherapy’ kwa watoto
11/12/2024 Duración: 01minNchini Rwanda Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa msaada wa UNICEF Switzerland na Liechtenstein wamesaidia tiba kwa njia ya mazoezi kuponya watoto wenye ulemavu wa viungo. Selina Jerobon anasimulia akiangazia mtoto mmoja, Joshua.
-
11 DESEMBA 2024
11/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia ripoti ya WHO inayohusu malaria, na juhudi za UNICEF na wadau wake nchini Rwanda za kusaidia watoto waliozaliwa na ulemavu kuweza kutembea. Makala tunakupeleka nchini Yemen na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Takwimu mpya zilizotolewa leo na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, zinaonyesha kuwa ingawa takriban wagonjwa bilioni 2.2 wa malaria na vifo milioni 12.7 vya ugonjwa huo vimeepukwa tangu mwaka 2000 bado ugonjwa huo unaendelea kuwa tishio kubwa la kimataifa la afya hususan katika Kanda ya Afrika ya WHO na hivyo juhudi zaidi zahitajika kuutokomeza.Nchini Rwanda Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa msaada wa UNICEF Uswisi na Liechtenstein wamesaidia tiba kwa njia ya mazoezi kuponya watoto wenye ulemavu wa viungo. Selina Jerobon anasimulia akiangazia mtoto mmoja, Joshua.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Yemen kusikia yaliyojiri baada ya ndoto za vijana kuelekea Saudi Arabia kuishia Yemen.Na mashinani mashinani hivi majuzi d
-
WHO: Ingawa vifo milioni 12.7 vya malaria vimeepukwa juhudi zaidi zahitajika kutokomeza gonjwa hilo
11/12/2024 Duración: 01minTakwimu mpya zilizotolewa leo na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO zinaonyesha kuwa ingawa takriban wagonjwa bilioni 2.2 wa malaria na vifo milioni 12.7 vya ugonjwa huo vimeepukwa tangu mwaka 2000 bado ugonjwa huo unaendelea kuwa tishio kubwa la kimataifa la afya hususan katika Kanda ya Afrika ya WHO. Taarifa ya Flora Nducha inafafanua zaidi.
-
UNFPA: Elimu ndio ufunguo wa kutokomeza FGM Kenya
10/12/2024 Duración: 05minLeo ikiwa ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu tunaelekea Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa ya idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA kutokomeza janga hilo. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya amefuatilia kuhusu suala hilo na kwa undani zaidi ungana naye ..
-
10 DESEMBA 2024
10/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunaelekea nchini Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na UNFPA na wadau mbalimbali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka nchini Namibia.Baada ya serikali ya Bashar Al-Assad kupinduliwa na kuibuka kwa taarifa za baadhi ya nchi duniani kuanza kusitisha mchakato wa kushughulikia maombi ya Wasyria waliokuwa wameomba hifadhi kuokoa usalama wa maisha yao pindi hali ilipokuwa tete nchini mwao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linaendelea kutoa wito kwa mataifa yote kufungua milango, kuwapa hifadhi na ulinzi raia wa Syria wanaotafuta usalama. UNHCR imeahidi pia mara tu hali ya Syria itakapokuwa wazi zaidi, itatoa mwongozo kuhusu mahitaji ya ulinzi kwa Wasyria walioko hatarini.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekaribisha mchango wa dola za Marekani milioni 22 kutoka shirika la Korea Kusini la Ushir
-
WHO na UNICEF wafikisha chanjo ya polio kwenye maeneo yasiyofikika ya West Pokot Kenya
09/12/2024 Duración: 02minShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya kenya na wadau wengine wa afya hivi karibuni wamezindua kampeni ya chanjo ya polio katika jamii ya wafugaji na wakulima ya kaunti ya West Pokot Mashariki mwa Kenya ambako mara nyingi ni vigumu kufikiwa. Flora Nducha amefuatilia kampeni hiyo na kutuandalia taarifa ifuatayo..
-
UN yaahidi kusaidia Wasyria kuiboresha nchi yao
09/12/2024 Duración: 01minKufuatia jana Wananchi wa Syria kutwaa madaraka kutoka kwa uongozi uliowatawala kwa mabavu kwa zaidi ya miongo mitano, viongozi wa Umoja wa Mataifa wameendelea kutoa wito wa kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa fursa ya mustakabali bora kwa kuzingatia haki za binadamu, uhuru na haki kisheria. Taarifa iliyoandaliwa na Anold Kayanda inaeleza zaidi.
-
Simfahamu baba yangu, natamani nimfahamu kwani nakosa upendo wake
09/12/2024 Duración: 03minWafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanazuiwa kutumia chakula, fedha au vitu vingine kwa ajili ya kushawishi ngono kutoka kwa mtu mwingine. Operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zinachukua hatua zaidi kuepusha ukosefu huo wa maadili , lakini bado visa hivyo vinaendelea kutokea. Katika baadhi ya matukio, watoto waliozaliwa kupitia uhusiano wa aiana hiyo wanasalia nyuma kwenye mazingira ya mizozo ambako baada ya baba zao kumaliza kuhudimia, huondoka na kubaki bila baba. Makala hii ya leo inamulika kisa kimoja cha mama na mtoto ambao wamesalia baada ya mlinda amani aliyempatia ujauzito mama husika kuondoka na kurejea nchini mwake. Msimulizi wako ni George Musubao
-
09 DESEMBA 2024
09/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Syria, na kampeni ya chanjo ya polio huko Pokot nchini Kenya. Makala tunasalia huko huko DRC na mashinani tnakwenda nchini Msumbiji, kulikoni?Kufuatia jana Wananchi wa Syria kutwaa madaraka kutoka kwa uongozi uliowatawala kwa mabavu kwa zaidi ya miongo mitano, viongozi wa Umoja wa Mataifa wameendelea kutoa wito wa kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa fursa ya mustakabali bora kwa kuzingatia haki za binadamu, uhuru na haki kisheria.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya kenya na wadau wengine wa afya hivi karibuni wamezindua kampeni ya chanjo ya polio katika jamii ya wafugaji na wakulima ya kaunti ya West Pokot Mashariki mwa Kenya ambako mara nyingi ni vigumu kufikiwa.Makala tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikiliza mama ambaye alipatiwa ujauzito na mlinda amani wa Umoja wa Mataifa na kisha kujifungua mtoto ambaye anasimulia kadhia ya kutomf
-
Asante WFP kwa kusambaza dawa za kuua magugu mmebadii maisha yangu: Mkulima Catherine Wanjala
06/12/2024 Duración: 03minMradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP wa kusambaza dawa ya bioherbicide ya kuuwa magugu kwenye mashamba ya mtama na mahindi kwa wakulima wa Kakamega magharibi mwa Kenya umekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima kama Catherine Wanjala ambaye magugu hayo yalimuharibia mazao na hata kuilazimisha familia yale kulala njaa wakati mwingine kwa kukosa chakula. Kwaa ufafanuzi zaidi ungana na Flora Nducha katika makala hii.
-
Miaka 15 ya Mkataba wa Kampala kuhusu wakimbizi wa ndani au IDPs, wito watolewa kwa nchi kuidhinisha na kutekeleza
06/12/2024 Duración: 02minKatika kuadhimisha miaka 15 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika chini Muungano wa Afrika, Kamishna Mkuu Msaidizi wa Ulinzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Ruven Menikdiwela na Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za Wakimbizi wa ndani Paula Gaviria Betancur wametoa kauli ya pamoja ya kupongeza Muungano wa Afrika kwa maono haya ya mbali na pia kuzisihi nchi zote barani Afrika kuutekeleza mkataba huo muhimu. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
-
06 DESEMBA 2024
06/12/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika, na siku ya kimataifa ya kujitolea inayotupeleka nchini DRC. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Zambia, kulikoni?Katika kuadhimisha miaka 15 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika chini Muungano wa Afrika, Kamishna Mkuu Msaidizi wa Ulinzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Ruven Menikdiwela NA Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za Wakimbizi wa ndani Paula Gaviria Betancur wametoa kauli ya pamoja ya kupongeza Muungano wa Afrika kwa maono haya ya mbali na pia kuzisihi nchi zote barani Afrika kuutekeleza mkataba huo muhimu.Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya kujitolea kwa ajili ya amani na maendeleo, tunakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mmoja wa wafanyakazi wa kujiolea wa Umoja wa Mataifa anaelezea uzoefu wake na ni kwa nini anajivunia kufanya kazi hiyo.M
-
André Bifuko - Najivunia kupatia wengine ujuzi wangu kwa ajili ya amani na maendeleo
06/12/2024 Duración: 01minDunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya kujitolea kwa ajili ya amani na maendeleo, tunakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mmoja wa wafanyakazi wa kujiolea wa Umoja wa Mataifa anaelezea uzoefu wake na ni kwa nini anajivunia kufanya kazi hiyo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.