Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
08 SEPTEMBA 2025
08/09/2025 Duración: 09minHeko MONUSCO na FARDC kwa kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha: LacroixSiku ya kimataifa ya kujua kusoma na kuandika.WHO yatoa orodha ya dawa muhimu duniani.
-
MINUSCA washiriki kutoa elimu ya usalama barabarani CAR
05/09/2025 Duración: 02minKila mwaka,Wizara ya Uchukuzi na Usafirishaji wa Anga nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwa msaada wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MINUSCA,huandaa kampeni za usalama barabarani. Na hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo,Bangui, MINUSCA kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya Ndani ISF wameungana kupambana na ajali za barabarani zinazoongezeka kila uchao,doria ya pamoja imefanyika kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara. Sabrina Saidi anatujuza zaidi....(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Natts ....ongeza hii; katikaa mitaa ya Banguimji mji mkuu wa CAR pisha nikupishe ni nyingi. Kufuatia ongezeko la ajali za barabarani,zinazopoteza maisha ya watu kila uchao, kikosi cha polisi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSCA kimeendesha doria ya pamoja ya usalama kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya nchi hii (ISF) katika mji mkuu BanguiOperesheni hii iliyofanyika tarehe 4 mwezi Septemba,mwaka huu imelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki za abiria maarufu
-
UNICEF: Mateso kwa watoto wa Gaza ni bayana
05/09/2025 Duración: 02minSasa twende Gaza, hii ni hadithi ya maisha, ya watoto wa Gaza wanaokabiliana na baa la njaa, hofu, na kuporomoka kwa kila kitu kinachowaweka hai. Ni hadithi inayoelezwa kupitia macho ya wale wanaoshuhudia mateso kila siku wakiwemo madaktari, akina mama, na wahudumu wa kibinadamu wanaopiga kengele ya tahadhari. Miongoni mwa wahudumu hao ni Tess Ingram afisa mawasiliano wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ofisi ya Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Flora Nducha anasimulia alichokishudia(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Tess aliyefunga safari na kushuhudia hali halisi Gaza akizungumza na waandishi wa habari kutoka mji wa Al Mawasi amesema mwenye macho haambiwi tazama na alichokishuhudia ni cha kutisha kwani jiji hilo sasa linazidi kuzama kwenye lindi la baa la njaa, vituo vya lishe vimefungwa, familia zinalia na kuhaha na watoto wanakufa kila uchao bila msaada.(Tess Ingram- Sheillah)“Jiji la Gaza, kimbilio la mwisho kwa familia za Kaskazini, linakuwa mahali ambapo utoto hauwezi kuishi.&
-
WMO: Ubora wa hewa duniani wazidi kuzorota japo kuna nafuu Asia na Ulaya
05/09/2025 Duración: 02minWakati mabilioni ya watu wakiendelea kuvuta hewa chafu inayosababisha zaidi ya vifo vya mapema milioni 4.5 kila mwaka, wataalamu wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa leo Ijumaa (5 Septemba) wamebainisha madhara ya chembe ndogo ndogo za moshi kutoka katika moto wa nyika ambazo husafiri umbali mrefu duniani kote. Philip Mwihava na maelezo zaidi.(Taarifa ya Mwihava)“Ubora wa hewa hauheshimu mipaka,” anasema Lorenzo Labrador, Afisa wa Kisayansi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO). Anaendelea kueleza kwamba, “moshi na uchafuzi unaotokana na moto wa nyika katika msimu huu wa kihistoria katika Rasi ya Iberia tayari umepatikana Ulaya Magharibi, kwa hiyo athari zake hazibaki tu kwenye Rasi ya Iberia, bali zinaweza kusambaa kote barani Ulaya.”Akiwasilisha taarifa ya WMO kuhusu Hewa Safi na Tabianchi, ambayo inakusanya data kutoka vyanzo mbalimbali vya kimataifa, leo jijini Geneva, Uswisi Bwana Labrador ametangaza mwendelezo wa mwenendo wa kuzorota kwa ubora wa hewa duniani.Ameonyesha ramani ya d
-
05 SEPTEMBA 2025
05/09/2025 Duración: 09minKaribu kusikiliza jarida la Habari za Umoja wa Mataifa ambapo leo tunakuletea taarifa kuhusu hali ya hewa na athari za moto wa nyika, tutaelekea Gaza kusikia kutoka kwa mashuhuda wa madhila wayapatayo watoto na wananchi wa Gaza na kisha tutaelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako wanaendesha mafunzo ya usalama barabarani.
-
Jifunze KIswahili: Maana ya methali "MASIKINI HANA MIIKO"
04/09/2025 Duración: 43sLeo katika jifinze Kiswahili mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "MASIKINI HANA MIIKO"
-
04 SEPTEMBA 2025
04/09/2025 Duración: 10minKatika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa leo Flora Nducha anakuletea-Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani UN-HABITAT lataka wakusanyaji na wachakataji wa taka watambuliwe kwani ni uti wa mgongo wa kuhakikisha mazingira safi na salama mijini-Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameipongeza Papua New Guinea kwa kuwa kisima cha kuvuna hewa ukaa na kuzitaka nchi za G-20 kuwajibika katika kudhibiti mabadiliko ya tabianchi-Nchini Mali, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ameonya juu ya kuzorota zaidi kwa hali ya haki za binadamu. -Na leo katika jifunze Kiswahili Je wafahamu maana ya methali "MASIKINI HANA MIIKO"? basi msikilize mtaalam wetu Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani
-
UNMISS yaimarisha doria jimboni Tambura Sudan Kusini
03/09/2025 Duración: 03minKatika jitihada za kuimarisha amani na usalama katika maeneo yaliyoathiriwa na machafuko ya kikabila nchini Sudan Kusini, Umoja wa Mataifa kupitia Ujumbe wake wa amani nchini humo UNMISS wameendelea kuimarisha ulinzi na kuongeza doria za magari usiku na mchana huko Greater Tambura katika jimbo la Equatoria Magharibi.Sabrina Saidi anaangazia juhudi za UNMISS katika kuhakikisha hali ya usalama inarejea na wananchi waliokimbilia katika kambi za wakimbizi kusakama usalama wanarejea makwao.TAARIFA YA SABRINA SAIDI)NAT...Video ya UNMISS inaanza kwa kumulika doria zinazofanywa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko katika kaunti ya Greater Tambura katika jimbo la Western Equatoria, kusini-magharibi mwa nchi ya Sudan Kusini karibu na mipaka ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.Tangu mwaka 2021, mizozo ya wenyewe kwa wenyewe, umeendelea kugharimu maisha ya watu wengi na kuwalazimu maelfu kuyakimbia makazi yao.Wananchi waliokumbwa na hofu wamekuwa wakijificha vichakani, wengine
-
Wakimbizi Nyarugusu wahamasika kufanya usafi
03/09/2025 Duración: 02minShirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC wanahakikisha wakimbizi wanaoishi katika kambi za wakimbizi za mkoani Kigoma Magharibi mwa Tanzania ikiwemo kambi ya nyarugusu wanapata huduma muhimu za maji na usafi kupitia ushirikiano wa viongozi wa wakimbizi. Huduma hizo zimekuwa changamoto kubwa katika kambi za wakimbizi zikichangiwa na ukata wa ufadhili. Flora Nducha na taarifa zaidi (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoibuka Burundi mwaka 2015, na baadaye mapigano kuighubika upya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, maelfu ya watu walikimbia na kuvuka mpaka kuingia Tanzania. Leo, wengi wao wanaishi katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kama vile Mtendeli, Nduta, na Nyarugusu.Lakini maisha kambini hayajakuwa rahisi. Kwa ufadhili mdogo, familia zinapata shida kupata huduma za msingi kama maji safi, makazi, na elimu.Hapo ndipo Shirika la UNHCR, na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC, wanapoingia. Tangu mwa
-
UN yatumia kila mbinu kuhakikisha inawafikia waathirika wa tetemeko Afghanistan
03/09/2025 Duración: 02minJuhudi kubwa za msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililoipiga Afghanstan mwishoni mwa wiki, zimeendelea leo huku watoa misaada wakikabiliwa hali ngumu ya kuwafikia wanaohitaji msaada kutokana na Barabara kuzibwa na kukatika kwa mawasiliano. Anold Kayanda na taarifa zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Taarifa mpya kutoka kwa timu za tathmini za Umoja wa Mataifa zilizofanikiwa kuwafikia waathirika katika wilaya ya milimani ya Ghazi Abad jana Jumanne kwa njia ya miguu, zimeweka wazi umuhimu wa kuendeleza tena kwa haraka msaada wa kibinadamu.Salam Al-Jabani kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) mjini Kabul anasema, “jambo la dharura ni kuwatoa watu chini ya vifusi na Watu wanasema wanachohitaji kwa haraka ni msaada wa kuwazika waliofariki dunia na kuwatoa waliofunikwa.”UNICEF inasema watoa misaada wake walilazimika kutembea kwa saa mbili ili kuwafikia watu na bado kuna vijiji ambavyo ili kuvifikia unahitaji kutumia saa sita hadi saba na hata helikopta hazijafanikiwa kufika huko
-
03 SEPTEMBA 2025
03/09/2025 Duración: 09minKaribu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa, hii leo utasikia juhudi zinazofanyika kusaidia wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan. Kutoka barani Afrika utasikia juhudi za kulinda raia wa Sudan Kusini wanaoathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe huko jimboni Tambura na kutoka nchini Tanzania utasikia msaada kwa wakimbizi walioko magharibi mwa taifa hilo.
-
Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno "URAIBU NA HITARI”.
02/09/2025 Duración: 01minKatika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua tofauti ya "URAIBU NA HITARI”.
-
02 SEPTEMBA 2025
02/09/2025 Duración: 10minJaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa FAO Mjini Morogoro, uliokutanisha viongozi wa Serikali kutoka katika Taasisi zinazojihusisha na udhibiti na usalama wa chakula. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na changamoto za afya ya akili kama vile msongo wa mawazo na mfadhaiko, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO. Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema nchi wanachama zinapaswa kushughulikia tatizo hilo kwa “Kuwekeza katika afya ya akili, kwani kuwekeza kwa watu, jamii na uchumi ni uwekezaji ambao hakuna nchi inayoweza kuupuuzia.”Umoja wa Mataifa umetuma salamu za rambirambi na pole kwa wananchi wa sudan kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua mkubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa ambayo imesababisha maafa katika kijiji cha Tarsin huko Jebel Marra nchini Sudan mwishoni mwa wiki.Nchini Afghanistan am
-
IFAD imejengea uwezo wanawake Nepal ambao awali walighubikwa na ukata
29/08/2025 Duración: 01minNchini Nepal suala la waume kwenda kusaka ajira nje ya nchi na kuacha wake zao wakihaha kukimu familia zao katika mazingira ambamo wanawake wanakuwa hawana uthabiti wa kiuchumi limeanza kupatiwa muarobaoni. Je ni kwa vipi? Assumpta Massoi anakufahamisha zaidi.
-
Guterres aonya dhidi ya kurejea kwa majaribio ya silaha za nyuklia duniani
29/08/2025 Duración: 01minKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres ametoa wito kwa mataifa yote kuridhia mara moja Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya Silaha za Nyuklia (CTBT), akisema “ni wakati wa kunyamazisha mabomu kabla hayajasikika tena.”
-
29 AGOSTI 2025
29/08/2025 Duración: 09minJaridani leo tunaangazia Majaribio ya Nyuklia, na machafuko nchini Sudan Kusini. Makala tunakwenda nchini Nepal na mashinani tunasalia huko huko Sudana Kusini, kulikoni?Dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa yakupinga Majaribio ya Nyuklia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa onyo kali kuhusu kuongezeka kwa hatari za nyuklia kufuatia mvutano wa kisiasa unaondelea duniani na amehimiza kuridhiwa kwa mkataba wa kupiga marufuku majaribio hayo ya kinyuklia.Maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao huko Tambura, jimbo la Equatoria Magharibi, tangu ghasia zilipozuka upya mwaka 2021 nchini Sudan Kusini. Hadi leo, wengi wao bado wanaishi kambini bila chakula cha uhakika, huduma za afya wala usalama huku wanawake na watoto wakibeba mzigo mkubwa zaidi wa mateso hayo.Makala tunakwenda nchini Nepal kumulika suala la waume kwenda kusaka ajira nje ya nchi na kuacha wake zao wakihaha kukimu familia zao katika mazingira ambamo wanawake wanakuwa hawana uthabiti wa kiuchumi limeanza kupatiwa muarobaoni.Na katika m
-
Wanawake wa Tambura Sudan Kusini: Tumechoshwa na mzunguko wa vita tunachotaka ni amani
29/08/2025 Duración: 03minMaelfu ya watu wameyakimbia makazi yao huko Tambura, jimbo la Equatoria Magharibi, tangu ghasia zilipozuka upya mwaka 2021 nchini Sudan Kusini. Hadi leo, wengi wao bado wanaishi kambini bila chakula cha uhakika, huduma za afya wala usalama huku wanawake na watoto wakibeba mzigo mkubwa zaidi wa mateso hayo. Kupitia video ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNIMSS Flora Nducha anamulika kauli za baadhi ya wanawake waathirika wanaosihi katika kambi ya wakimbizi wa ndani.
-
Maji ni Uti wa mgongo kwa jamii kote duniani - Stephen Tai
28/08/2025 Duración: 05minWiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mtendaji huyo anayeanza kwa kujitambulisha, anazungumza na Kelvin Keitany wa radio washirika Radio Domus nchini Kenya.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MKWIJI!.
28/08/2025 Duración: 01minKatika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWIJI!
-
28 AGOSTI 2025
28/08/2025 Duración: 09minJaridani leo tunakuletea mada kwa kina, wiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mengine ni kama yafuatayo.Ukraine ambapo leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameungama na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kulaani vikali mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani droni yaliyofanywa na Urusi usiku kucha kuamkila dhidi ya miji ya Ukraine na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto, na pia kuharibu majengo ya kidiplomasia jijini Kyiv. Amesisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao yanakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu, akitaka yakome mara moja na kurudia wito wake wa kusitisha mapigano ili kuelekea amani ya kudumu itakayoheshimu uhuru wa watu, uhuru wa kitaifa na mipa